Msanii Black Rhino ambaye ni ndugu wa Mbunge Mteule wa jimbo la Mikumi Joseph Haule au Profesa Jay, amewataka viongozi waliochaguliwa na wananchi kuwaongoza, watekeleze matakwa ya wananchi na endapo hawatafanya hivyo watakutwa na laana ya wananchi hao.
Black Rhino ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba iwapo jamii ikikupa dhamana sio suala dogo hivyo waende kupiga kazi.
"Mi ninachoweza kusema ni kwamba kwa wasanii wote au vijana ambao wamepewa dhamana na wananchi, ninacho waasa tu ni kwamba watu waende kupiga kazi, kwa sababu jamii ikiamua kukupa dhamana ni kitu kizito sana, dhamana ya umma ni jambo la kuliheshimu sana", alisema Black Rhino.
Black Rhino aliendelea kusema...."Wanasema duniani hapa kuna laana ya wazazi, lakini umma unaweza ukakulaani wewe, iwapo kama walikuwa na imani na wewe wakakupa dhamana ya kuwasaidia, wakakuamini wakakupigia kura, alafu unaenda kuchukua jukumu hilo ukajifunaisha tumbo lako binafsi, basi elewa kuna laana kubwa ambayo utaipata, sawa tu na laana ya mzazi", alisema Black Rhino.
Profesa Jay anakuwa msanii wa pili kuingia Bungeni akiwa kama mbunge mteule, baada ya Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu ambaye ni mbunge wa jimbo la Mbeya mjini.