Akiongea na waandishi wa habari mjini Sumbawanga mwenyekiti wa Chadema wa mkoa wa Rukwa Bw Zeno Nkoswe, amesema licha ya kutoridhishwa na uteuzi wa Aida Kenani kuwa mbunge wa viti maalumu kutoka mkoa huo wa rukwa, pamoja na makao makuu ya chama kupewa taarifa mapema kuwa kiongozi huyo hivi sasa amekuwa msaliti, kwani mara tu baada ya kura za maoni amekuwa anakipigia debe chama cha TLP, lakini pia kutotekelezwa kwa ahadi ya kuwalipa mawakala zaidi ya 1,000 waliosimamia uchaguzi kwenye vituo mbalimbali, pia imekuwa sababu ya wao kujiuzuru nafasi zao.
Kwa upande wake katibu wa Chadema wa mkoa wa Rukwa Bw Ozem Chapita, akitoa ufafanuzi wa hatua hiyo amesema uteuzi wa mtu ambaye anaonekana ni msaliti, kunaweza kukaathiri hata uwezekano wa chama hicho kilichoshinda viti kumi kati ya tisa vya udiwani, kuweza kuiendesha halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga kwa kuwa na meya wa manispaa, kwa kushindwa kupata kura za kutosha.