Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijobisimba
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo Bisimba amepata ajali mbaya leo jijini Dar na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
Bi Hellen Kijo Bisimba anaendelea kupatiwa matibabu na vipimo katika hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam.
Gari alilopata nali ajali Dk. Kijobisimba.
Dk. Kijo Bisimba amepata ajali akiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 yenye namba za usajili T 336 CTT.
Kaimu mkurugenzi wa kituo hicho Imelda Urio amesema kuwa Bi Hellen Kijo Bisimba na wenzake watatu waliokuwemo katika ajali hiyo wanaendelea vizuri na wengine wanaweza kuruhusiwa kurudi nyumbani.