Jeshi la polisi mkoani Pwani linamshikilia Mganga Mfawidhi Ramadhan Mtambo wa zahanati ya kijiji cha Mkongo Kaskazini kilichopo Wilayani hapa kwa tuhuma za kupatikana na dawa za binadamu bila kibali.
Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, kamanda Jafari Mohamed alisema Mganga huyo alikamatwa na mwenyekiti wa kijiji hicho Mussa Mohammed Sungu majira ya saa 9:31 Alasiri katika kituo cha Afya Kibiti siku ya jumatatu.
Alisema Mganga huyo alikamatwa na boksi kumi na tatu za dawa za kutibu Malaria aina ya Artemether and Lumefantrine maarufu kwa jina la Mseto kukiwa na dozi 390 za kutibu ugonjwa huo.
Kamanda Jafari alisema dawa hizo zilikuwa na thamani ya shilingi 975,000 za kitanzania na zilikuwa zimepelekwa katika zahanati ya kijiji hicho siku chache kabla ya tukio.
Alisema, Mganga huyo alipohojiwa ni wapi alipokuwa akizipeleka dawa hizo, Dr Ramadhani Mtambo alijibu alikuwa akizipeleka katika kituo cha Afya Kibiti kwa ajili ya kubadilishana dawa hizo na dawa za kushusha msukumo wa damu (B.P) Alisema baada ya kutokea mvutano kati ya Mganga huyo na Mwenyekiti wa kijiji hicho, kulipelekea Mganga huyo kumshambulia Mwenyekiti huyo kwa bakora baada ya kubaini mpango wake umeharibika.
Kamanda Jafari alifafanua kuwa kufuatia mvutano huo askari polisi waliitwa ambapo walifika na kumkamata Mganga huyo hadi Kituo cha Polisi Kibiti ambapo baada ya kuupekuwa mfuko aliokuwa nao walikuta una dawa hizo za kutibu malaria box kumi na tatu.
Kamanda Jafari alieza kuwa walilazimika kumuita Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Kibiti Dr Jones Chagi kwa ajili ya kuja kutoa maelezo ya madai yaliyotolewa na Mganga huyo, lakini alikana hakuwa na makubaliano yoyote na Mganga ya kubadilishana dawa.
Akizungumzia mkasa huo, Mwenyekiti huyo Mussa Mohammed Sungu alisema alimshitukia mganga huyo huenda amebeba dawa hizo hivyo kulazimika kumfuatilia kwa pikipiki hadi alipomkuta katika eneo la Corecu Kibiti.
Alisema baada ya kumuona alisimamisha pikipiki yake kisha kuanza kumhoji na baadaye kukata fimbo na kumshambulia maeneo mbalimbali mwilini mwake, kabla ya kutaka kukimbia na kuutelekeza mfuko huo ambapo watu walijitokeza na kumsaidia kumkamata mganga huyo.