Unknown Unknown Author
Title: MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA HAYATI SIMON KAMILLIUS MEMBE.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Baadhi ya waombolezaji wakishiriki kwenye ibada ya mazishi ya Marehemu Simon Kamillius Membe iliyofanyika katika kijiji cha Rondo huko L...
Mazishi ya Simon Kamillius Membe
Baadhi ya waombolezaji wakishiriki kwenye ibada ya mazishi ya Marehemu Simon Kamillius Membe iliyofanyika katika kijiji cha Rondo huko Lindi Vijijini tarehe 7.10.2015.
Mazishi ya Simon Kamillius Membe
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Benard Kamillius Membe akitoa neo la shukrani kwa viongozi wa serikali, Chama Cha Mapinduzi na wananchi waliojitoa kwa hali na mali katika kufanikisha mazishi ya marehemu kaka yake Bwana Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia huko India tarehe 3.10.2015.
Mazishi ya Simon Kamillius Membe
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapa pole wana familia ya Marehemu Simon Kamillius Membe mara baada ya kuhudhuria ibada ya mazishi iliyofanyika huko Rondi, Lindi Vijijini tarehe 7.10.2015.
Mazishi ya Simon Kamillius Membe
Baadhi ya waombolezaji wakipita mbele ya jeneza ulimolazwa mwili wa Marehemu Simon Membe aliyefariki dunia huko India tarehe 3.10.2013.
Mazishi ya Simon Kamillius Membe
Mheshimiwa Benard Membe akitoa heshima za mwisho wakati wa kuuaga mwili wa marehemu kaka yake Ndugu Simon Camillius Membe mara baada ya kufanyika ibada ya mazishi huko Kijijini Rondo tarehe 7.10.2015.
Mazishi ya Simon Kamillius Membe
Maandamano ya kwenda kuulaza mwili wa Marehemu Simon Membe kwenye nyumba yake ya milele huko kijijini Rondo katika wilaya ya Lindi.
Mazishi ya Simon Kamillius Membe
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Simon Membe wakati mwa mazishi katika Kijiji Rondo huko Lindi.
Mazishi ya Simon Kamillius Membe
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Benard Membe akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu mdogo wake ndugu Simon Membe wakati wa mazishi yake huko Rondo TAREHE 7.10.2015.
Mazishi ya Simon Kamillius Membe
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia huko India tarehe 3.10.2015.

PICHA NA JOHN LUKUWI.

About Author

Advertisement

 
Top