Unknown Unknown Author
Title: TEMEKE WATINGA FAINALI AIRTEL RISING STARS
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mchezaji wa timu ya Ilala Rukia Annaph (kushoto) akichuana vikali na mchezaji wa timu ya Temeke Christina Daudi katika mchezo wa nusu fa...
Airtel Rising Stars
Mchezaji wa timu ya Ilala Rukia Annaph (kushoto) akichuana vikali na mchezaji wa timu ya Temeke Christina Daudi katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi September 17. Temeke ilishinda 2-1)
Airtel Rising Stars
Mchezaji wa timu ya Ilala Tumaini Michael (Kulia) akimtoka mchezaji wa timu ya Temeke Shamimu Hamis katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi September 17). Temeke iliibukana na ushindi wa magoli 2-1)

Na. Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Temeke girls jana walifanikiwa kutinga hatua ya fainali, baada ya kuwagaragaza majirani zao wa Ilala kwa kuwafunga mabao 2-1 katika muendelezo wa michuano ya U-17 ya Airtel Rising Stars,mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Ilala ambao walionekana kuumiliki mpira kwa kiasi kikubwa sana katika kipindi cha kwanza walifanikiwa kuandika bao mnamo dakika ya 1 baada ya Tumaini Michael kuachia shuti na kutinga wavuni huku kipa wa Temeke akiwa hana la kufanya.

Al manusra Ilala wapate bao la pili manmo dakika ya 20 baada ya Tumaini Michael tena kupiga mpira wakichwa ambao ulipaa kidogo langoni mwa Temeke.

Katika kipindi cha pili,Temeke walionekana kucharuka huku wakicheza kwa kasi kubwa, na ndipo mshambuliaji wa timu hiyo, Shamimu Hamisi mnamo dakika ya 40, alipomalizia kwa umaridadi mpira uliotemwa na kipa wa Ilala na kuukwamisha moja kwa moja wavuni na kusawazisha goli.

Temeke waliofanikiwa kuandika goli la pili mnamo dakika ya 61 kupitia kwa Asia Juma na kudidimiza matumaini ya Ilala kutinga hatua ya fainali.

Baada ya mchezo huo kocha wa Ilala Omari Bwezi alisema: “Tumekubali matokeo,wachezaji wangu walicheza vizuri kipindi cha kwanza lakini walionekana kuchoka sana kipindi cha pili na kuwapa nafasi ya kutawala wenzetu na ndio maana tukafungwa”.

Naye kocha wa Temeke Daudi Siang’a alisema: “Vijana wangu walifuata niliyowalekeza wakati wa mapumziko na waliporudi uwanjani walifanya nilichowaeleza na hatimaye tukapata matokeo”.

About Author

Advertisement

 
Top