Unknown Unknown Author
Title: LINDI NA MTWARA WAOMBWA KUKINYIMA KURA CHAMA CHA MAPINDUZI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea. Wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara, wameombwa kukinyima kura Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu ujao, k...
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.
Wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara, wameombwa kukinyima kura Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu ujao, kwa madai kuwa hakiwapendi na kimejenga chuki nao bila sababu.
Lindiyetu blog News
Wito huo ulitolewa jana mjini hapa, na mratibu wa uchaguzi wa CUF-Chama Cha Wananchi, kanda ya kusini, Nurdin Msati kwenye mkutano wa kampeni ya kumnadi mgombea wa ubunge jimbo la Nachingwea anayepitia chama hicho, Jordan Membe..

Msati alisema wananchi wa mikoa hiyo hawana sababu ya kukipenda Chama Cha Mapinduzi kwa madai kuwa hakiwapendi kuliko wakoloni ambao waliwajengea reli ambayo iling'olewa na CCM kwasababu ya chuki isiyo na sababu.

Alisema lengo la kuwaondoa wakoloni lilikuwa nikujitawala nakuwa na maendeleo. Hata hivyo TANU ambayo ilizaa CCM iliondoa matarajio ya watu wa mikoa hii kwa kuondoa hata mema yaliyofanywa na wakoloni kwa ajili ya wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara.
"Wazee wetu kwakuamini kuwa wakiwaondoa wakoloni watakuwa na maendeleo, waliwaeleza kama ili waondoke nilazima watumie uchawi basi wanao kwani miti ya kutengeneza uchawi ilikuwepo, kama nifedha wanazo na walikuwa tayari kuchangishana" kama ni maombi haikuwa kikwazo kwasababu walikuwepo mashehe na mapadri, mwisho wa siku wazungu waliondoka hata hivyo watawala kwa kuwachukieni wakaondoa hata vile vilivyotengenezwa na wakoloni," alisema Msati.

Alibainisha kuwa kitendo cha kutowaletea maendeleo wananchi wa mikoa hii hakina tofauti na kuvunja mkataba halali uliofanywa baina ya wananchi na serikali. Hivyo hawana sababu ya kukikumbatia chama ambacho hakiwathamini na chenye chuki nao.

Ofisa wa chama hicho toka makao makuu, Mahinda Saburi Mahinda alimtabiria ushindi mgombea wa urais anayepitia UKAWA, Edward Lowassa kwa madai kuwa anakubalika na watu wa dini zote na wasio na dini, ambao wote watampigia kura.
"Lipumba na Slaa walikuwa wanakwamishwa na dini zao kiasi cha wananchi wengine kuwa na wasiwasi nao, lakini Lowassa anapendwa na watu wa dini zote na hata wasioamini dini wanampenda "hata wana CCM wanaojitambua wanampenda na watampigia kura, ametuunganisha watu wa dini na makabila yote," ali asema Mahinda.

Aliongeza alisema mgomboa wa urais kupitia CCM, Dk John Magufuli hawezi kukomesha ufisadi kwasababu yupo ndani ya chama chenye mfumo wa ufisadi. Akimfananisha na dereva wa gari iliyozama kwenye tope anayewahaidi abiria kuwa ataikwamua akiwa ndani ya gari hiyohiyo wakati anajua wanaoweza kuisukuma na kuiondoa ni watu walionje.

Mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa chama hicho anayewakilisha wilaya ya Nachingwea, Manaki Athuman alisema CCM hakiaminiki kwasababu hakielewi kinasimamia nini. Badala yake kimekuwa kikiamini na kuhubiri mambo ambayo hakitendi. Ikiwamo itakadi ya ujamaa na kujitegemea ambayo inaamini na kuihubiri, lakini imekumbatia na kuendesha nchi kwa mfumo wa ubepari.

Kwaupande wake Membe aliwaomba wananchi kumpigia kura ili awawakilishe kwani anaouzoefu wa kupigania na kutetea maslahi yao. Chama hicho kimefikisha mikutano 21 ya kampeni ya kumnadi mgombea wake wa ubunge tangu kianze rasmi kampeni zake.

About Author

Advertisement

 
Top