Unknown Unknown Author
Title: MAGUFULI APIGWA NA BUTWAA NYOMI LA GEITA, AAHIDI KUSHUGHULIKIA MATATIZO YA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika...
Kampeni CCM. 2015
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Kalangalala mjini Geita leo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Mgombea Urais Huyo amewaambia wananchi wa Geita kuwa mara atakapoingia Ikulu, moja ya changamoto anazotarajiwa kuzipa kipaumbele ni pamoja na suala la kutatua mgogoro wa wachimbaji madini wadogo wadogo.

Magufuli ameasema kuwa akiingia madarakani atawapa maeneo wachimbaji wadogo wa madini nchini ikiwa ni pamoja na kuwakopesha mitaji na kuwapa vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi zao pamoja na mafunzo kwa ajili ya kuboresha uchimabaji wao ili uwe wa kisasa zaidi na kupandisha kiwango cha ufanisi wa kazi zao za uchimbaji.

Dkt. Magufuli leo amehutubia mikutano katika miji ya Runzewe wilayani Bukombe, Katoro wilayani Chato na Geita mjini akiendelea na kampeni zake za kwaomba wananchi kumpa kura za ndiyo ili aweze kuingia Ikulu na kuwafanyia kazi Watanzania kama kiongozi na Amiri Jeshi mkuu wa Tanzania.

Kampeni CCM. 2015
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwanadi Wagombea Ubunge wa jimbo la Busanda Mh.Lolensia Bukwimba na Dkt Meedad wa Chato mapema mchana huu alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita, kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,katika mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.Dkt Magufuli atahutubia jioni ya leo mjini Geita kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Kampeni CCM. 2015
Wananchi wa Runzewe wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa kampeni.
Kampeni CCM. 2015
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita na mgombea ubunge wa jimbo la Geita vijijini Ndugu Joseph Kasheku a.k.a King Msukuma akihutubia malefu ya wananchi wa Geita mjini kwenye mkutano wa kampeni wa Urais,ambapo Ndugu Joseph aliwaomba wakazi wa Geita na vitongoji vyake kumchagua Dkt John Pombe Magufuli awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka.
Kampeni CCM. 2015
Magufuli Style ilitikisa pia ndani ya Geita kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt John Pombe Magufuli jioni ya leo.
Kampeni CCM. 2015
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwapokea mlemavu wa ngozi Albino Lazaro Malendeka kushoto ambaye alikuwa mtumishi wa kikundi cha Red Briged cha Chadema baada ya kujiunga na CCM mjini Geita leo na William Mabula Msalaba aliyekuwa mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Geita.
Kampeni CCM. 2015
Wananchi wa Katoro wakiushangilia msafara wa Dkt Magufuli alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.

About Author

Advertisement

 
Top