Unknown Unknown Author
Title: BARUANI AVIFUNGUKIA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, ATAKA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YA WATU HAWA..!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mgombea Ubunge jimbo la Lindi Mjini(CUF) Salam Baruani amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwafutilia na kuwachukulia hatua za kisheria...
Mgombea Ubunge jimbo la Lindi Mjini(CUF) Salam Baruani amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwafutilia na kuwachukulia hatua za kisheria mabalozi wa chama cha Mapinduzi wanachukua namba za vitambulisho vya kupigia kura kinyume na sheria za tume ya uchaguzi.
Salam Baruani
Hayo ameyasema wakati alipokuwa anazungumza na wakazi wa kata ya wairles kwenye mkutano wa Kampeni wa kuomba ridhaa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Baruani alisema kuwa anaviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao na kutenda haki ili kampeni ziendelea kufanyika kwa amani na utulivu kwa kuwazibiti mabalozi wa ccm wanaokiuka taratibu za tume ya uchaguzi.

Alisema kuibuka kwa kundi la mabalozi wa CCM kupita kuchukua namba za kadi ya kupigia kura ni jambo ambalo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani hivyo ni vyema vyombo vya ulinzi na usalama vikachukua taadhari juu ya jambo hilo kabla halijaanza kusababisha vurugu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wa wilaya Lindi Yahaya Nawanda alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema ofisi yake haijapata malalamiko yoyote kuhusiana na hoja hiyo.

About Author

Advertisement

 
Top