Na. Ahmad Mmow. Lindi
Kiasi, neno kiasi ni dogo sana kulitamka. Lakini uzito wake ni mkubwa kuliko kulitamka kinywani. Hakika wenye kulifanyia kazi kwa vitendo wananufaika nalo sana. Bali wasio lifanyia kazi na kulidharahu wamejikuta wanapata hasara kubwa na hata matatizo.
Kiasi, neno kiasi ni dogo sana kulitamka. Lakini uzito wake ni mkubwa kuliko kulitamka kinywani. Hakika wenye kulifanyia kazi kwa vitendo wananufaika nalo sana. Bali wasio lifanyia kazi na kulidharahu wamejikuta wanapata hasara kubwa na hata matatizo.

Miongoni mwa waliolipuuza neno hili kwa siku za hivi karibuni ni mzee wangu Kingunge Ngombale Mwiru. Mzee wangu huyu alimpenda waziri mkuu mstahafu Edward Lowassa kupita kiasi. Alijiapiza kumtaka aingie ikulu kupita kiasi. Alisema na kumwagia sifa kupita kiasi. Nasasa baada ya Lowassa kukatwa jina lake anasema na kulia kupita kiasi. Tena anaharibu na kukiharibu chama chake kupita kiasi.
Bila shaka wapo watu wanaanza kumchukia kupita kiasi. Bila shaka mkakati wake wakuungwa mkono katika hayo anayodhani yanaweza kumsaidia yeye na anayemlilia unaweza kushindwa kupita kiasi. Nimatokeo ya kufanya mambo kupita kiasi.
Niliwahi kueleza kwenye moja ya maandiko yangu kwa nia njema kabisa, kutokana na mwenendo na dalili za mheshimiwa Lowassa kutopitishwa na chama chake. Kauli za viongozi wa juu wa chama hicho ambazo zilikuwa na kiasi. Zilionesha zitakuwa na kishindo kikuu. Ingewezekana wapi aliyeshika mpini akatwe na kisu bali aliyeshika kwenye makali awe salama? Mzee Kingunge pamoja na kula chumvi nyingi inaelekea alilisahau hilo. Ndipo nilitoa angalizo la kuwataka watu wenye matumaini kupita kiasi akiwamo mzee Kingunge kujiandaa kisaikolojia pindi wanaye muunga mkono atakapo katwa.
Kitendo cha kutoshinda wagombea ambao walikuwa na matarajio makubwa nilikifananisha na sunami. Nikaeleza wazi kwamba sunami haita acha chochote bali vilio na ukiwa. Hakika yametokea na yametimia. Bila shaka historia imeandikwa na haitafutika. Tuliyaona mafuriko, nayo yamewajeruhi wengi, lakini sunami ni funga kazi. Nilisema mchezo wasiasa ni mtamu kwa mwenye kufanikiwa. Lakini ni mchungu na mbaya kwa asiyefanikiwa.
Unatabia ya kukupatia mashabiki na marafiki kwa muda mfupi na ghafla. Lakini unatabia ya kukuacha mpweke na mkiwa ghafla. Tunasikia nakusoma kwenye vyombo vya habari kwamba waliokuwa wanamuunga mkono mheshimiwa Lowassa wanakihama Chama Cha Mapinduzi. Hata hivyo mheshimiwa Lowassa na mzee Kingunge wanaendelea kubaki ndani ya CCM. Maana yake nikwamba wanachama hao wameamua kuwaachia chama chao (mzee Kingunge na Lowassa) ambao wamebaki wasijue hatima yao hadi sasa. Kifupi wamebaki wakiwa, wakati mzee Kingunge akibaki kama mfariji mkuu. Mzee wangu aliaminiwa ndani ya CCM kupita kiasi, naye akajiamini kupita kiasi ndiyo maana alisema na anaendelea kusema kupita kiasi kama anavyokimbiwa na kuchukiwa kupita kiasi.
Hapa palipofikia ilikuwa nimuafaka awe wakwanza kuhama kabla ya wanaohama sasa lakini kupenda chama na mtu kupita kiasi kunasababisha andelee kubaki ndani ya CCM, ingawa sasa hakipendi na anakiona kichungu kupita kiasi. Alimpa matumaini Lowassa kupita kiasi hanabudi kumfariji kupita kiasi maana asipofanya hivyo hataeleweka kabisa. Inakuwaje sasa, kubaki CCM kwa mwenendo wa sasa nijaribio lenye utata kwani hawezi kuaminika tena na watu anaowaona nitatizo ndani ya chama. Na ndio hao walioshika mpini na wanamuunga mkono John Magufuli. Waliofanya mambo kwa kiasi walau wana amani ingawa nao hawafurahii yaliyotokea. Kuendelea kupiga kelele haimsaidi mzee Kingunge wala anayempigania, bali waliowengi kama sio wote wanamuona anapiga kelele za mfamaji tu. Aibu hailalii mwaka, nauenda bila kelele zake ingeanza kupungua kama sio kumalizika kabisa. Lakini kwa mwenendo huu wa sasa ni dhahiri aibu ya kushindwa italalia mwaka.
Maana mzee Kingunge hataki watu wasahau yaliyojiri Dodoma. Tunajua kwamba kuwa mwanachama wa chama siojela jela. Unaweza kuhama tu, inakuwaje mzee Kingunge uendelee kupiga kelele ukiwa ndani ya CCM, unasubiri nini kuondoka, si uhame uwaachie chama chao?
Hata unayempigania mwambie muhame, maana mmebaki wakiwa, wafuateni wafuasi wenu ili tuone CCM kama kitakufa au kitaendelea kuwa hai. Kuendelea kupayuka kupita kiasi hakukusaidi wewe wala unayempigania kupita kiasi.
Nauliza tena unangoja nini ndani ya CCM umelazimishwa? Kwani CCM nijela? Mbona hayati mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa CCM siyo mama yake. Kinachokufanya uendelee kung'ang'ana ndani ya CCM wakati unajua hakifai ni nini!.
Tags
MAKALA