MACHESTER UNITED imefungua rasmi maongezi na Paris St-Germain juu ya kumpiga bei winga wake mwenye thamani ya pauni milioni 60 Angel Di Maria. Daily Star la Uingereza limefichua kuwa mkurugenzi msaidizi wa michezo wa PSG Olivier Letang alipaa kwenda London wiki iliyopita kuanza mazungumzo na mtendaji mkuu wa United Ed Woodward.

Woodward amerejea England akitokea kwenye ziara ya Manchester United ya mechi za maandalizi ya msimu mpya huko Marekani na kukutana kwa siri na Letang siku ya Jumatatu. PSG iko tayari kulipa pauni milioni 40 kwa winga huyo wa kimataifa wa Argentina, lakini United inataka pesa inayokaribiana na kitita cha pauni milioni 60 walicholipa kwa Real Madrid msimu uliopita.
Maongezi zaidi yatachukua nafasi wiki hii kukiwa na matumaini ya kukamilika kwa dili hilo ingawa United imesisitiza kuwa inataka kiasi kisichopungua pauni milioni 50.
Maongezi zaidi yatachukua nafasi wiki hii kukiwa na matumaini ya kukamilika kwa dili hilo ingawa United imesisitiza kuwa inataka kiasi kisichopungua pauni milioni 50.
United imetumia pauni milioni 80 kwa kuwanunua Bastian Schweinsteiger, Morgan Schneiderlin na Memphis Depay kiangazi hiki huku pia ikitarajiwa kuongeza mshambuliaji mwingine kabla dirisha la usajili halijafungwa.
Chanzo:: Saluti5
Tags
SPORTS NEWS