MSHALE WA MLIMA ILULU:: MEMBE NA MWANDOSYA TUMEWASIKIA, WENGINE VIPI?

Na.Ahmad Mmow.
Wapendwa, mimi sio miongoni mwa wapiga madebe wala mapipa. Tena kwa sasa mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa. Uamuzi wangu huu wa kutokuwa na chama unanifanya niwe huru na amani sana. Siwashawishi wasomaji wangu msiwe wanachama wa vyama vya siasa, bali mimi kutokana na sababu ambazo ikimpendeza Mungu nitawaeleza siku nyingine sitaki kuwa mwanachama. 

Kwangu vyama ni kama mpira, hasa kwa watu ambao wanadhani vyama vinathamani kuliko wao. Nakwamba wao nikwa ajili ya vyama nasiyo vyama kwa yao. Uzezeta, undondocha, uchizi! Kwanini mtu wa aina hiyo chama kisiwe ni sawa na kongwa! Nimetangulia kueleza hayo kwa haya nitakayo yaeleza. Isije kuonekana natumwa au mfuasi wa mtangazania fulani, miongoni mwa watangaza nia.
Waliojitetea
Tumesikia mengi katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. Watangazania karibu wote wa upinzani na chama tawala, ajenda yao kubwa nikupambana na ufisadi. Hata hivyo kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ambaye kama Unasoma maandiko yangu naomba anisaidie kujua huyo kiongozi mkuu ninani. Maana vyama vingine viongozi wake wakuu ni wenyeviti wa taifa. 

Baadhi ya nchi viongozi wake wakuu wanaitwa marais, mawaziri wakuu, wafalme nk. Ni kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo aliyeweka mjadala mezani Kuhusu ufisadi. Zitto alisema watangazania wa urais, hasa wanaopitia Chama Cha Mapinduzi wanahoja za kuwajibu wananchi kutokana na tuhuma mbalimbali za ufisadi. Sababu watangazania hao hawajakanusha tumuhuma hizo. Hivyo wananchi wameubaki bila majibu, nakuendelea kubaki na kiu ya kupata ukweli wanamna walivyohusika na tuhuma hizo.Hakika Zitto aliweka mjadala mezani.

Tayari watangazania wawili kati ya wanne waliotajwa na Zitto kuwa wanamaswali ya kujibu, wamejitokeza kujibu na kukanusha tuhuma zinazozungumzwa juu yao. Hongera Membe na Mwandosya kusimama hadharani. Ndivyo inavyotakiwa kufanywa na viongozi. Tuhuma zikanushwe haraka zinapokushukia. Ingawa majibu ya profesa Mwandosya nimepesi kuliko maswali.

Zitto nilimsikia pale uwanja wa Ilulu Lindi. Maswali ya msingi yalikuwa nikwanini mashirika yaliuzwa kwa bei ya kutupwa. Ikiwamo kitengo cha makontena katika bandari ya Dar, shirika la reli na kampuni ya simu. Hoja ya pili ni tuhuma kwamba walionunua TTCL ndio waliogharamia masomo ya mwanawe profesa. Zitto hakulaumu kuuzwa ambako kulipewa jina la ubinafshaji. 

Majibu ya profesa Mwandosya hayakujibu swali hilo. Pia hajakanusha tuhuma ya pili ya mwanawe kugharamiwa masomo na 'wadosi' walionunua TTCL. Pole profesa kama nitakuwa nimekukosea. Kama ulishajibu hayo naomba radhi sana. Nisamehe sana mzee. Iwapo hujajibu, basi endelea kuwajasiri na kujibu maswali hayo.

Mtangazania mwingine ni waziri wa mambo ya nje, Bernad Membe. Hakika kwa akilizangu za jioni na usiku
na uelewa mdogo nadiriki kusema amejibu tuhuma na amepangua kwa hoja zenye mashiko nazenye kubeba ushahidi. Iwapo kashfa ya Membe ilikuwa ni hiyo pekee, basi anayosababu ya kujiita msafi. Membe ameweka wazi kuwa jambo analotuhumiwa nalo hakuhusika kwa namna yoyote. 

Akieleza bila chembe ya hofu ushahidi ulijitokeleza. Kama jambo hilo lilifikishwa na kushuguli na muhimili mmoja kati ya mitatu. Jambo hilo lilifikishwa na kushugulikiwa na mahakama kwa kufuata taratibu zote. Namwisho mahakama ilitoa uamuzi ambao hadi sasa hakuna aliyeupinga. Hayo nimaelezo ya Membe. Iwapo kama nikweli nidhahiri hakuhusika. Hongera Membe kama aliyoeleza ndiyo ukweli wenyewe.

Kitendo kilichofanywa na profesa Mark Mwandosya na Benard Membe ni cha kupongezwa. Hata hivyo bado wa heshiwa Lowassa, Dr Magufuli wapo kimya, vipi! Watanzania tunakiu ya kuwasikia mkikanusha kutohusika na tuhuma mnazotuhumiwa nazo. Kanusheni kwa hoja zenye mashiko kama alivyofanya Membe. Pamoja na Lowassa na Magufuli, lakini pia watanzania tunahamu ya kusikia jaji Augustine Ramadhan ukikanusha tuhuma ya kuwa mwanachama wa CCM ukiwa jaji mkuu. Hamu ya watanzania kukusikia jaji Ramadhan imekolezwa na katibu wa idara ya itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye. Katibu huyo amesema CCM haina watangazania wa urais wakuokoteza, bali ni makada wenye sifa zote na watiifu kwa chama hicho. Wanaitambua misingi, itakadi na malengo yake. Nisifa ambazo jaji Ramadhan unazo. Hakika mwanachama aliyejiunga na chama hicho katika muda mfupi siyorahisi kuwa na sifa hizo. Nawe simama ueleze kama hausiki na tuhuma hizo ambazo hatari yake nikuuwa demokrasia. Simama mchana kweupe jaji utueleze watanzania kama wewe sio muuwaji wa demokrasia.

Hofu nikwamba ukiwa rais huwezi kuwatendea haki watu wasiokiamini chama chako. Utaua demokrasia ambayo ustawi na uhai wake ni muhimu kwetu. Msisubiri mteuliwe na chama chenu muwe wagombea ndipo mtujibu, tunataka sasa. Kama mnasubiri kuteuliwa ndipo mjibu tutakuwa hatuwaelewi na tutawakataa. Hamuwezi kuwa marais mkiwa na makandokando. Jipeni moyo muweze kujibu maswali yetu. Msikimbilie kutaka kutuongoza tu, kwani sisi ni watu wala siyo mizigo. 

Tuonane siku nyingine wapendwa.
0757115673 na 0717924695.
Previous Post Next Post