MARCELO ASAINI MKATABA MPYA NA REAL MADRID, SASA KUBAKIA HADI 2020

Klabu ya Real Madrid imemuongezea mkataba beki wake wa kushoto mbrazil Marcelo kwa misimu miwili zaidi, klabu hiyo kubwa ya Hispania imetangaza leo mkataba huo mpya.
Marcelo
Hivyo mchezaji huyo atakuwa amejitia kitanzi cha kusalia Bernabeu hadi mwaka 2020. Taarifa kutoka Real Madrid zinasema mkataba huo mpya wa Marcelo utadumu hadi mwezi wa sita mwaka 2020, hivyo kumuongezea misimu mitano kuichezea klabu hiyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, alijiunga na klabu hiyo mwaka 2007 kwa ada ya Paundi Mil.6 akitokea klabu ya nchini brazil inayoitwa Fluminense. Akiwa katika ushirikiano mzuri na kipa na Nahodha wa timu hiyo Iker Casillas na Makamu nahodha Sergio Ramos, Mchezaji huyo ameweza kucheza mechi 320 kwa miaka Tisa katika klabu hiyo.
Klabu hiyo imebainisha kuwa wameamua kumpatia mkataba wa muda mrefu beki huyo ili kulinda uwepo wake klabuni hapo kutokana na Uvumi uliopo miezi kadhaa sasa baada ya wanaohusishwa kwa Maveterani wa klabu hiyo Casillas na Ramos kutaka kuondoka klabuni hapo. Casillas na Ramos wamejiunga  leo hii na wachezaji wenzao kushiriki katika Mafunzo ya mazoezi ya kwanza na kocha mpya Rafael Benitez katika viwanja vya klabu hiyo unaoitwa Valdebebas.
Benitez alichukua mikoba ya aliyekuwa Kocha wa timu hiyo Carlo Ancelotti kufutwa kazi baada ya kukosa taji lolote kwa msimu wa 2014/2015.
Previous Post Next Post