Katika mahojiano hayo Wema Sepetu amezungumza kuhusu ishu ya kuwa na mahusiano na boyfriend wa Lina alisema "...Huwezi amini hizo habari si za kweli kwasababu tulikuwa tunafanya project zinakuja ila nimeshangashwa kuona kwanini Lina ameenda on air kwenye kipindi na kuzungumza hizo habari kuwa natembea na boyfriend wake naomba watu waelewe kwamba sikweli…”
Hivi sasa Wema Sepetu yupo mkoani Singida kwenye maandalizi ya kuchukua fomu ya kugombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi kupitia Viti Maalumu. Pia Wema amejiandikisha katika Daftari la wapigakura mkoani humo kwa kuwa ndio Mkoa atakao gombea na pia Mama mzazi ni mzawa wa mkoa huo. Hivi sasa kazi aifanyayo ni ya ushawishi kwa vijana wajitokeze katika kujiandikisha kwenye daftari hilo la kudumu la wapiga kura.
Tags
HABARI ZA WASANII