MSHALE WA MLIMA ILULU:: DR. MAHIGA, NAYE YALEYALE YA MJANE NA MGANI

Na.Ahmad Mmow.
"Ninawasiwasi chama hakitanipitisha, maana sina mpango wa kutoa fedha za kuhonga kama wengine" ndani ya chama hiki huwezi kupata uongozi bila kutoa rushwa...mimi sitahonga katika mchakato mzima", mwisho wa kunukuu.
Dr Augstine Mahiga
Wapendwa,hayo maneno niliyoyanukuu ndiyo yamenusukuma nipate cha kuandika. Hayo nimaneno machache sana, lakini kama utatuliza ubongo nakudurusu walau mara mbili, bila siaka utapata cha kujifunza. Lakini pia utapata maswali na mwisho utapata majibu. Maneno hayo ni ya mmoja kati ya wanachama wengi wa Chama Cha Mapinduzi waliotangazani ya kuomba ridhaa ya Chama hicho wateuliwe au wapitishwe kugombea urais kupitia chama hicho. 
Mwenye maneno hayo ni msomi bobezi na aliyepata kuiwakilisha nchi yetu katika mataifa ya mbali kwa nafasi ya ubalozi, Dr Augstine Mahiga. Mwanachama huyo mwaminifu na mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi.

Kupitia maneno hayo anatusaidia na kuungana na wengine wanaokishambulia chama hicho na viongozi wake. Ndio! Dr Mahiga ameungana na wengine kukishambulia chama ambacho anasema hata hama katika uhai wake wote hata kama nicha wapenda rushwa. Sababu ya kutohama kuendelea kubaki kwenye chama ambacho viongozi na wachama wake wakawaida wanapokea na kutoa rushwa ameitaja.
Sababu kubwa ni mbili.
Mosi; Ndicho chama kilichomlea. 
Pili; Ndicho chama kilichopigania uhuru. 
Hizo ndiyo sababu zinazomfanya msomi huyo aking'ang'anie chama hicho mithili ya kupe juu ya ngozi. Hatari kwelikweli. Niliamini sababu hizo zinaweza kutolewa na watu wa saizi yangu mimi kielimu, siyo kwa msomi wa daraja yake. Nilijidanganya! Kumbe tupo wengi.
Dr, amesema chama hicho huwezi kushinda bila rushwa. Tunatambua kuwa kabla ya majina ya waombaji halmashauri na mkutano mkuu nilazima yachujwe wajumbe wa vikao anayomba vya awali. Ikiwamo sekretarieti na na kamati kuu, ni vikao vinavyowahusisha viongozi wakuu wa chama hicho. Ambao pia wanaingia kwenye kikao cha halmashauri kuu na mkutano mkuu. Balozi Mahiga anaposema katika chama hicho kama haunafedha huwezi kupitishwa, maana yake hata viongozi wakuu wanakula rushwa. Nituhuma mzito kwakweli ambayo inazidi kutuaminisha kuwa ndani ya chama hicho hakuna msafi. 
Hakuna lugha nyingine zaidi ya hiyo. Kama ndani ya chama hicho hakuna msafi, maana yake hata watangazania hawana usafi pia. Si wamekulia humohumo jamani! Maana yake ni tatizo la kimfumo. Haiwezekani mtu asiye na fedha asiwe nanafasi ya kupitishwa ikawa nitatizo la mtu mmoja mmoja mmoja. Bali nilakimfumo. Hata hivyo bado anasema akipitishwa na kuwa rais atapambana na rushwa. Duh! sasa atapitishwa nanani tena wakati ameshasema bila kuhonga hawezi kupitishwa. Nayeye anasema hataki kuhonga. Sasa atapitaje tena jamani ili awe rais aweze kupambana na rushwa? Au wenzangu wenye akili nyingi mnauonaje mkorogo huu.
Kwangu mimi natoatafsiri kwamba balozi Mahiga anaichukia rushwa wakati amejiandaa kutoa rushwa. Maana haiwezekani aape hatatoa rushwa na wakati huo anataka kupambana na rushwa akiwa rais, wakati anajua bila kutoa rushwa hawezi kupitishwa. Hivyo hawezi kuwa rais, kwani njia ya kumfikisha huko itakuwa imejifunga.
Yote kwa yote na yeye itabidi atoe rushwa ili apitishwe. Nandipo anapoamini akiwa rais atapambana na rushwa. Ingawa nayeye atakuwa ametumia njia hiyohiyo hadi kuwa rais. Amesema vikao vitende haki, nijambo lisilowezekana na niutetezi mfu anaojaribu kupoozesha kauli yake kali. Sina shaka na ninavyodhani, nikutokana na sababu nyepesi alizozieleza za kuendelea kubaki ndani ya chama ambacho rushwa ni mfumo wake.
Balozi kuendelea kuwa ndani ya chama hicho nijibu kuwa ameridhika na yanayotendeka. Hayati baba wa taifa aliwahi kusema kuwa ccm siyo mama yake. Maana yake ni kwamba hayati baba wataifa alikuwa tayari kukitosa chama hicho iwapo angeona kinapoteza misingi na malengo ya kuanzishwa kwake. Miongoni mwa misingi hiyo ni rushwa.
Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa. Niliamua kubaki bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa baada ya kuhisi ubabaishaji uliomo kwenye vyama. Hata hivyo nilibaki kuwa mshabiki wa CCM kwa ajili ya malengo yake, hata hivyo kwa kadri siku zilivyokuwa zinayoyoma nikagundua hata nako kunaimani bila matendo. Nakwakauli ya hayati baba wa taifa nikaona niunge mkono kwa vitendo kwamba chama sio wazazi wangu. Ni kaweka boli chini. Hata hivyo bado nakumbuka kuwa moja ya msingi wa chama cha mapinduzi katika ahadi zake ni rushwa kwangu mwiko, sitatoa wala kupokea. Kwakuwa wenyewe wanasema CCM inanuka rushwa, nadhani ni muda ambao baba wataifa angekuwa hai angekitosa.
Ndipo unaweza kujiuliza baba wataifa na balozi Mahiga ninani alisitahilinkusema hawezi kukihama? Hayati mwalimu na baba wa taifa wapi na wapi! Masihara kabisa. Miaka yote nilikuwa nawapuuza wapinzani kwa kukinasibisha chama hiki na rushwa na kaka yake ufisadi. Lakini uchaguzi wa mwaka huu ambao kwa wanachama wa ccm wanaoutaka urais wanaona sawa na mchezo karibu na kumalizika inapofunguliwa milango ili wasiona pesa za viingilio waweze kuingia(fungulia mbwa) ambapo watu wanasukumana kuingia ili walau wakaone sekunde za kadhaa kabla ya mchezo kumalizika.
Ndipo tunawasikia kwa vinywa vyao bila kulazimishwa ila uchu wa urais wanatamka yaleyale ambayo mimi nilikuwa nayapuuza kwa kuwaona ni wabangaizaji na waganga njaa kupitia siasa. Hivi ni kweli kazi anayofanya mzee Kinana ni usanii? 
Tusemeje kama sio usanii ilihali baadhi ya makada wake wanaotaka urais wanasema bila ya bila rushwa hawawezi kupitishwa? Mzee Kinana na Nape wanaingia karibu kwenye vikao 
vyote vyenye uwezo wa kumpitisha mgombea urais kupitia chama hicho. Na makada wanasema bila rushwa huwezi kupitishwa. Kwa mantiki hiyo mzee Kinana, mwenyekiti, makamo na wengine wote wanakula rushwa.
Balozi hajasema ni kikao gani cha maamuzi na akina nani wanakula rushwa ili kuwapitisha wagombea. Sidhani kama ninayonia ya kuwaondoa kwenye tuhuma hiyo mzito na kubwa kuwahi kutamkwa. Bado najiuliza hivi hawa watu wanakitakia mema chama hiki au wamekata tamaa na sasa wameaua kukirarua na kukiharibu ili wakose wote. Maana haiingii akilini utake ridhaa ya chama hichohicho na utamke maneno kama hayo.
Kinachoonekana hapa kwa akilizangu nusu na robo ni tukose wote. Achuliwae kila uchao hana maisha marefu. Tusubiri tuone.
MUNGU IBARIKI TANZANIA. 0757-115973/ 0717-924695
Previous Post Next Post