
Kaimu Mdhibiti UKIMWI mkoa wa Lindi DR. EDGER MLAWA, Aakizungumza na waandishi wa Habari pamoja na Maafisa wa AGPAF (HAWAPOPICHANI) ambao walipotembelea Hospitali ya Mkoa ya Sokoine katika zoezi la uhamasishaji wa watoto wenye VVU kubaki na Kuhudhuria kwenye vituo na kuendelea kutumia dawa.
Na.Abdulaziz Ahmeid, Lindi.
Imeelezwa kuwa kasi ndogo ya upimaji wa maambukizi ya watoto wenye maambukizi ya VVU mkoani Lindi inasababishwa na baadhi wazazi ambao hawataki kuwaeleza ukweli watoto wao walioambikizwa. Hayo yalielezwa jana na kaimu mdhibiti UKIMWI (kaimu mratibu) wa mkoa wa Lindi, Dr Edgar Mlawa, alipokuwa anazungumza na timu ya waandishi wa habari pamoja na maafisa wa shirika lisilo la kiserikali la Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundition (EGPAF) linaloshugulika na kuzuia maambukizi ya virusi ya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda mtoto, matibabu na matunzo kwa watu wanauishi na vya UKIMWI(VVU) linalofadhiliwa na shirika la misaada la watu wa Marekani(USAID) CDC.
Alisema wazazi na walezi wengi hawawaelezi watoto wao kuwa wameathirika, badala yake wamekuwa wakieleza wanywe dawa bila ya kuwaeleza sababu.
"kwakuwa hawaambiwi sababu watoto hao wamekuwa hawatumii dawa kama inavyotakiwa na hawaendi kwenye vituo vinavyotoa huduma za matibabu na matunzo, na kusababisha idadi ya watoto waliosajiliwa na kutumia dawa ni ndogo chini ya lengo,"alisema Dr Mlawa.
Alisema lengo ni kuwasajili 15% hadi 20% ya watu wote wanaoishi na VVU waliosajiliwa. Hata hivyo ni watoto 8% tu kati ya watu wote walio sajiliwa katika mkoa huu. Alisema katika mkoa huu wenye jumla ya vituo 14 vya matibabu na uangalizi kwa wanaoishi na vvu, watu 25,086 wametambuliwa na kusajiliwa ambapo watu 15,466 wanapata matibabu.
"Hata hivyo ni watoto 1,922 tu ndio waliotambuliwa na kusajiliwa idadi ambayo ni sawa na 8% tu ya watu wote waliotambuliwa na kusajiliwa, kati ya wototo hao ni 1,179 wapo kwenye matibabu".
Alisema licha ya kutowaeleza, lakini pia wazazi wengi hawawapeleki kwenye vituo watoto wao wenye wanaoishi na VVU. Hivyo kusababisha watoto wengi kutopata matibabu, matunzo na ushauri wa namna ya namna ya kujitunza.
Mratibu huyo aliongeza kusema kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na tume ya taifa ya kudhibiti UKIMWI(TACTAIDS) hali ya maambukizi yamepungua. Kwani matokeo utafiti wa mwaka 2007/2008 yaliondesha kiwango cha maambukizi kilikuwa ni 3.8%, lakini utafiti wa 2011/2012 matokeo yalionesha kiwango cha maambukizi ni 2.9%. Ambapo maeneo yamjini yameendelea na maambukizi makubwa kuliko ya vijijini.
Mratibu huyo aliongeza kusema kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na tume ya taifa ya kudhibiti UKIMWI(TACTAIDS) hali ya maambukizi yamepungua. Kwani matokeo utafiti wa mwaka 2007/2008 yaliondesha kiwango cha maambukizi kilikuwa ni 3.8%, lakini utafiti wa 2011/2012 matokeo yalionesha kiwango cha maambukizi ni 2.9%. Ambapo maeneo yamjini yameendelea na maambukizi makubwa kuliko ya vijijini.
Aidha Dr Mlawa alisema ili kuwafanya watoto wanaoishi na VVU wapate ushauri na stadi za namna ya kujitunza, na kuwakutanisha pamoja. Zimeanzishwa klabu 14 (kambi) zenye jumla ya watoto 381.
Mratibu wa shuguli ya kijamii wa kituo cha uangalizi na matibabu(CTC) cha hosipitali ya Sokoine, Emerensiana Mtwiche. Alisema wanaume wengi katika mkoa huu hawajitokezi na kwenda kupima kwa hiari afya zao. Badala yake wanategemea matokeo ya vipimo wanavyopimwa wakezao na wapenzi wao. Kitendo ambacho hakitoi majibu sahihi ya afya zao.
Maafisa hao wa EGPAF ambao walitembelea zahanati, hospitali na vituo vya afya vilivyopo katika manispaa ya Lindi, kwa muda wa siku tatu walikuwa katika zoezi la uhamashaji ili watoto wanaoishi na vvu wabaki na kuhudhuria kwenye vituo na kuendelea kutumia dawa.
Tags
HABARI ZA KITAIFA