WAZAZI LINDI KIKWAZO UPIMAJI WA WATOTO WENYE VVU

Na.Abdulaziz Ahmeid,Lindi.
Imeelezwa kuwa kasi ndogo ya upimaji wa maambukizi ya watoto wenye maambukizi ya VVU mkoani Lindi inasababishwa na baadhi ya wazazi ambao hawataki kuwaeleza ukweli watoto wao walioambikizwa.
Jengo la Zahanati Ng'apa
Hayo yalielezwa jana na muuguza kiongozi wa kituo cha mafunzo na utoaji huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (CTC) katika hosipitali ya mkoa wa Lindi, Fatuma Khatau alipokuwa anazungumza na timu ya waandishi wa habari iliyokwenda katika hospitali hiyo.

Alisema wazazi wengi wamekuwa natabia ya kuwaficha ukweli watoto wao ambao wameathirika. Hivyo kusababisha watoto wengi wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI bila kupata huduma za matibabu.
"Idadi ndogo ya watoto waliosajiliwa nakupata huduma kwenye kituo chetu haimaanishi kama watoto wanaoishi na virusi vya UKIMWI,bali baadhi ya wazazi ambao ni wengi hawawaelezi ukweli kuwa wameathirika,badala yake wanaambia wanywe dawa bila kujua ni za ugonjwa gani," alisema Fatuma.

Muuguzi huyo ambaye alizizungumza na waandishi hao ambao walikuwa wamefuatana na maafisa wa shirika lisilo lakiserikali la EGPAF. Alisema hadi mwezi machi mwaka huu ni watoto 325 tu, kati ya watu 4080 waliosajili katika kituo hicho.
"kati ya watu hao wanaotumia dawa ni wanaume 780 wanawake 1536,kati ya hao wanaotumia dawa,watoto ni 194 tu" watoto wa kiume ni 98 na wakike ni 96," aliongeza kusema.

Alibainisha kuwa ili kuwafanya watoto hao wakutane mara kwa mara na kuwapatia mafunzo mbalimbali kuhusiana na tatizo la vvu na namna ya njia za kuishi kwa matumaini. Muuguzi huyo alisema wameanzisha klabu maalum ya watoto wanaoishi na maambukizo. Ambapo hadi sasa, kituo hicho kinawatoto 70. 

Naye mratibu wa shuguliza jamii wa kituo hicho, Eremensiana Mtwiche. Alisema wanaume wengi hawapendi kupima afya zao, badala yake wanategemea matokeo ya upimaji wanaofanyiwa wake zao na wapenzi wao.
"Hawa wanawake nirahisi sana kupimwa afya kwa sababu wanapokuja kuanza kliniki wakiwa wajawazito nilazima wapime pia na maambukizi ya VVU, hivyo wanaume wanategemea majibu ya vipimo vyo, jambo linaweza kusababisha wawe na hofu iwapo watasikia wake zao au wapenzi wao wameambukizwa wakati huenda hajapata maambukizo" vilevile wale ambao watasikia kuwa wapenzi wao hawaja ambukizwa wanaweza kujiona wapo salama lakini wanaweza kuwa wameambukizwa," alisema Mtwiche.

Timu hiyo ya waandishi ipo kwenye msafara wa maafisa wa shirika lisilo la kiserikali la EGPAF ambao wapo kwenye kampeni ya uhamasisha wa watoto wanye maambukizi ya VVU wabaki kwenye matumizi ya dawa na huduma.
Previous Post Next Post