RATIBA YA UCHAGUZI WA DOLA KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI ILIYOPITISHWA NA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA CHA TAREHE 23-24/05/2015

URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA TAREHE TUKIO
  1. 03/06/2015 hadi 02/07/2015 Kuchukua na kurudisha fomu. Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 02/07/2015 saa 10.00 jioni
  2. 03/06/2015 hadi 02/07/2015 Wadhamini
  3. 08/07/2015 Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili
  4. 09/07/2015 Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa
  5. 10/07/2015 Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa
  6. 11/07/2015 hadi 12/07/2015 Mkutano Mkuu
URAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR NA TAREHE TUKIO
  1. 03/06/2015 hadi 02/07/2015 Kuchukua na kurudisha fomu. Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 02/07/2015 saa 10.00 jioni
  2. 03/06/2015 hadi 02/07/2015 Wadhamini
  3. 04/07/2015 Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili - Zanzibar
  4. 05/07/2015 Kikao cha Kamati Maalum ya ya Halmashauri Kuu ya Taifa - Zanzibar
  5. 08/07/2015 Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili
  6. 09/07/2015 Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa
  7. 10/07/2015 Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kuteua mgombea Urais
UBUNGE NA TAREHE TUKIO
  1. 15/07/2015 hadi 19/07/2015 Kuchukua na kurudisha fomu. Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 02/07/2015 saa 10.00 jioni
  2. 20/07/2015 hadi 31/07/2015 Mikutano ya Kampeni kwa ajili ya kura ya maoni
  3. 01/08/2015 Kupiga kura ya maoni
  4. 02/08/2015 Kuandaa taarifa ya matokeo ya kura ya maoni
  5. 03/082015 Kikao cha Kamati za Siasa za Wilaya
  6. 05/08/2015 Kikao cha Kamati za Siasa za Mkoa
  7. 08/08/2015 Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa - Zanzibar
  8. 10/08/2015 Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa
  9. 11/08/2015 hadi 12/08/2015 Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kwa ajili ya uteuzi.
UJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI NA TAREHE TUKIO
  1. 15/07/2015 hadi 19/07/2015 Kuchukua na kurudisha fomu. Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 19/07/2015 saa 10.00 jioni
  2. 20/07/2015 hadi 31/07/2015 Mikutano ya Kampeni kwa ajili ya kura ya maoni
  3. 01/08/2015 Kupiga kura ya maoni
  4. 02/08/2015 Kuandaa taarifa ya matokeo ya kura ya maoni
  5. 03/08/2015 Kikao cha Kamati za Siasa za Wilaya
  6. 05/08/2015 Kikao cha Kamati za Siasa za Mkoa
  7. 08/08/2015 Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa - Zanzibar
  8. 10/08/2015 Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa
  9. 11/08/2015 hadi 12/08/2015 Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kwa ajili ya uteuzi
UBUNGE NA UJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI – VITI MAALUM - WANAWAKE NA TAREHE TUKIO
  1. 15/07/2015 hadi 19/07/2015 Kuchukua na kurudisha fomu. Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 19/07/2015 saa 10.00 jioni
  2. 02/08/2015 Mikutano Mikuu ya UWT Mikoa kupiga kura za maoni kwa wagombea 2 kwa kila mkoa.
  3. 03/08/2015 Baraza Kuu la Vijana Mkoa kupiga kura za maoni kwa wagombea wa Viti Maalum kundi la Vijana.
  4. 04/08/2015 Baraza Kuu la Wazazi Mkoa kupiga kura za maoni kwa wagombea Viti Maalum kundi la Wazazi.
  5. 05/08/2015 Kamati za Siasa za Mikoa kuandaa mapendekezo yatakayowasilishwa kwenye Baraza Kuu la UWT Taifa.
  6. 07/08/2015 Baraza Kuu la UWT kuandaa mapendekezo yatakayowasilishwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa.
  7. 08/08/2015 Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa
  8. 09/08/2015 Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
  9. 10/08/2015 Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa
  10. 11/08/2015 hadi 12/08/2015 Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kwa ajili ya uteuzi
UDIWANI WA KATA/WADI NA TAREHE TUKIO
  1. 15/07/2015 hadi 19/07/2015 Kuchukua na kurudisha fomu. Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 19/07/2015 saa 10.00 jioni
  2. 20/07/2015 hadi 31/07/2015 Mikutano ya kampeni kwa ajili ya kura ya maoni
  3. 01/08/2015 Kupiga kura ya maoni
  4. 02/08/2015 Kuandaa taarifa ya matokeo ya kura ya maoni
  5. 03/08/2015 Kikao cha Kamati za Siasa za Kata/Wadi
  6. 04/08/2015 Kikao cha Kamati za Siasa za Wilaya
  7. 05/08/2015 hadi 06/08/2015 Kikao cha Kamati za Siasa za Mikoa
  8. 07/08/2015 Kikao cha Halmshauri Kuu ya Mkoa kwa ajili ya uteuzi.
UDIWANI VITI MAALUM - WANAWAKE NA TAREHE TUKIO
  1. 15/07/2015 hadi 19/07/2015 Kuchukua na kurudisha fomu. Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 19/07/2015 saa 10.00 jioni
  2. 03/08/2015 Mikutano Mikuu ya UWT ya Wilaya kwa ajili ya kupiga kura ya maoni
  3. 04/08/2015 Kikao cha Kamati za Siasa za Wilaya
  4. 05/08/2015 hadi 06/08/2015 Kikao cha Kamati za Siasa za Mikoa
  5. 07/08/2015 Kikao cha Halmshauri Kuu ya Mkoa kwa ajili ya uteuzi.
MASHARTI KWA KILA NAFASI YA KUOMBEA UONGOZI
1. URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  • Kila mgombea ni lazima apate wadhamini 450 katika mikoa 15 walau 3 kati ya hiyo iwe ya Zanzibar.
  • Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa Taifa hawaruhusiwi kumdhamini mgombea Urais. 
  • Mwanachama haruhusiwi kumdhamini mgombea Urais zaidi ya mmoja.
  • Fomu ya udhamini ya wanachama ithibitishwe na Katibu wa CCM wa Wilaya kwa kupigwa muhuri wa Chama wa Wilaya husika.
  • Wanachama watakao mdhamini mgombea, uanachama wao uthibitishwe na Katibu wa CCM Wilaya husika na kupiga muhuri wa Chama.
2. URAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR
  • Kila mgombea ni lazima apate wadhamini 250 katika mikoa 3 kati ya hiyo angalau Mkoa mmoja toka Unguja na mmoja kutoka Pemba.
  • Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa Taifa hawaruhusiwi kumdhamini mgombea Urais.
  • Mwanachama haruhusiwi kumdhamini mgombea Urais zaidi ya mmoja.
  • Fomu ya udhamini ya wanachama ithibitishwe na Katibu wa CCM Wilaya kwa kupigwa muhuri wa Chama wa Wilaya husika.
  • Wanachama watakao mdhamini mgombea, uanachama wao uthibitishwe na Katibu wa CCM Wilaya husika na kupiga muhuri wa Chama.
3. UBUNGE
  • Kila mgombea atachangia gharama za safari za kampeni.
  • Kila mgombea atalazimika kuzingatia Maadili ya Chama Cha Mapinduzi na Miiko ya Uchaguzi wa ndani ya Chama.
4. UJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI
  • Kila mgombea atachangia gharama za safari za kampeni.
  • Kila mgombea atalazimika kuzingatia Maadili ya Chama Cha Mapinduzi na Miiko ya Uchaguzi wa ndani ya Chama.
5. UDIWANI WA KATA/WADI
  • Kila mgombea atachangia gharama za safari za kampeni.
  • Kila mgombea atalazimika kuzingatia Maadili ya Chama Cha Mapinduzi na Miiko ya Uchaguzi wa ndani ya Chama.

Aidha, wagombea wote wanatakiwa kuzingatia Kanuni za Chama Cha Mapinduzi.
Previous Post Next Post