PROF. IBRAHIMU LIPUMBA NA WAFUASI WAKE 30 WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Kesi inayomkabili mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF na wenzake 30, imeendelea katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu, Ambapo hakimu anayesikiliza shauri hilo amesema kesi hiyo inaweza kumalizika kwa wakati endapo mawakili wa upande wa watuhumiwa wataacha wakati wa kuuliza maswali kwa mashahidi wa upande wa serikali.
Ibrahimu Lipumba
Tofauti na siku nyingine mwenyekiti huyo wa chama cha wananchi CUF Prof Ibrahimu Lipumba aliwasili katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu Dar es Salaam mapema zaidi huku akifuatana na watuhumiwa wenzake katika kesi hiyo, Akitoa ushahidi wake mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya Kisutu, Bw Cyprian Mkeha, naibu kamishina wa jeshi la polisi Simon Siro aliyekuwa akiongozwa kutoa ushahidi huo na wakili wa serikali mkuu Bw. Bernald Kongola aliiambia mahakama kuwa mnamo tarehe 23.01.2015 ofisi yake ilipokea barua kutoka CUF ikitoa taarifa juu ya uwepo wa maandamano yakifuatiwa na mkutano wa hadhara uliopaswa kufanyika tarehe 27.01.2015 katika viwanja vya Zakiem Dar es Salaam.

Naibu kamishina huyo wa jeshi la polisi aliendelea kuieleza mahakama kuwa baada ya kupokea barua hiyo aliagiza vijana wake wa intelejinsia ilikufuatilia kuhusu mkutano huo ambapo aliletewa taarifa za kiintelejinsia na vijana hao wa jeshi la polisi kuwa kufanyika kwa mkutano huo kunge hatarisha hali ya amani na utulivu wa nchi kufuatia uwepo wa vitisho mbalimbali vya kigaidi.

Ambapo tareh 27.01.2015 aliwaandikia barua chama cha CUF ikiwataka kusitisha maandamano hayo pamoja na mkutano baada ya kubaini taarifa za kiintelegensia zilizohusu ugaidi ambapo kabla ya hapo alizungumza na Bw Abdull Kambaya kuhusu usitishwaji wa mkutano huo nakwamba walikubaliana kutofanya mkutano huo.

Hata hivyo mahakama imekubali kupokea vielelezo viwili vikiwemo barua iliyoandikwa na CUF wakiomba kufanya maandano na ile iliyoandikwa na kusainiwa na kamanda Siro juu ya kuutaka uongozi wa CUF kusitisha maandamano hayo, Kesi hii iliyochukua takribani saa tano za uendeshaji wake ililazimika kusimama kwa dakika kadhaa baada ya mabishano ya kisheria kutoka upande wa utetezi na upande wa mashitaka kuhusu kupokelewa au kutokupokelewa kielelezo cha kilichokuwa kikionyesha tarehe na muda wa barua ya katazo ilipofika katika ofisi za CUF, Lakini uwepo wa shauri hili linaathiri vipi shughuli za kisiasa za mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Lipumba.
Previous Post Next Post