Na.Ahmad Mmow. Lindi
Hatimae idadi ya watangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wanaongezeka, baada ya mtu ambaye kwa mtazamo wake anaipenda nchi yetu kuliko mtu yeyote, mtu ambaye anakipenda chama cha mapinduzi kuliko wanachama wote wa chama hicho, naye kutangazania.
Hatimae idadi ya watangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wanaongezeka, baada ya mtu ambaye kwa mtazamo wake anaipenda nchi yetu kuliko mtu yeyote, mtu ambaye anakipenda chama cha mapinduzi kuliko wanachama wote wa chama hicho, naye kutangazania.

Wapo waliomfuatia, lakini mimi Hapa ninazungumzia kada wa CCM na muumini wa siasa za chuki hasa kwa vyama upinzani, Mwigulu Nchemba.
Msema chochote bila kuangalia madhara kwa taifa alimoradi tu awafurahishe viongozi wa Chama na serikali. Mimi sikuamini niliposikia kwamba na yeye anaitamani nafasi ya urais.
Toba! nikaomba mungu apeperushie mbali wazo hilo la Mwigulu. Niwe mkweli ndugu zangu, Mwigulu simpendi awe rais na hafai kuwa rais. Miongoni mwa makosa tunayoweza kuyajutia ni kijana huyo mpenda sifa hata za kijinga kupewa nafasi hiyo inayomtaka mtu mwenye huruma, muungwana na mwenyebusara.
Mwigulu hana kabisa. Nimuongo, mshari na asiyechukua muda kutafakari athari na matokeo ya kauli na vitendo vyake kabla ya kutenda. Mtu wa aina hiyo ni hatari, hafai ataivuruga nchi. Nimemsikia na kumuona akitangaza nia ambapo alionesha kuzungumza kimlaka zaidi kana kwamba ameshakuwa rais.
Sifa za kijinga! Ujasiri wa kimamlaka unaotokana na kusukumwa na ukatili ni hatari. Mwigulu uhenda haamini kama nchi hii siyo mali ya Chama Cha Mapinduzi,ndiyo sababu anaujasiri wakuomba nafasi hiyo nakuzungumza kimamlaka kuliko waombaji wengine. Naamini angekuwa anajua kwamba nchi hii namali ya wote na wasio wanachama wa CCM asingethubutu kutaka kuomba nafasi hiyo ambayo inamtaka mtu anayeamini kuwa hata wasiowanachama wa CCM ni miongoni mwa wananchi wanaohitaji kuongozwa na yeye.Nchi ambayo inafuata mfumo wa siasa wa vyama vingi, na kwahiyo viongozi wa vyama hivyo nisawa na viongozi
wa CCM.
wa CCM.
Nitaeleza japo kwa ufupi. Tunajua kwamba nchi yetu inafuata demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Hivyo wote tunatakiwa kuwa waumini wa mfumo huu ambao ulirejeshwa rasmi mwaka 1992, kutokana na hekima na busara kubwa ya baba wa taifa, hayati mwalimu Julius Nyerere.
Mfumo ambao ulisitishwa mwaka 1965, ni baada ya uhuru wa Tanganyika. Hivyo nidhahiri tunatakiwa kuukubali kwa vitendo nasiyo kwa maneno.
Je,Mwigulu anaukubali na kuamini nchi hii inaamini katika mfumo wa vyama vingi vya siasa katika kusukuma mbele maendeleo ya nchi? Kwangu mimi nasema haamini hivyo, bali anaona vyama vya upinzani ni nuksi. Havitakiwi kuwepo, bila kujali kuwa muasisi wa mfumo huu ni yule aliyejaribu kujilinganisha nae kwenye hotuba yake ya kutangazania. Masihara. Mbona Mwilugulu na Nyerere nisawa nakumlinganisha shetani na malaika! kweli tumeamua kukufuru. Wote tumashahidi wakweli kijana huyu bila hata chembe ya huruma alivyowabambikia tuhuma mzito viongozi wa vyama vya upinzani, tuhuma ambazo mataifa ya nje yameanza kuiona nchi yetu sio salama tena. Alipotangaza mchana kweupe kuwa kunabaadhi ya wanasiasa ni magaidi. Tuhuma zilizosababisha Wilfred Lwakatare asote mahabusu bila sababu zenye ushahidi.
Yeye akijiapiza mbele ya bunge kuwa anaushahidi usio na chembe kuwa Lwakatare na wenzake ni magaidi. Bila shaka alifanya hivyo kwa maslahi ya chama chake na siyo ya nchi. Matokeo yake nchi yetu inatazamwa kwa jicho la hofu. Nilishangaa kusikia kunawatu wanalalamika kudhalilishwa kwa baadhi ya viongozi wetu wa serikali alipokuja rais wa Marekani, Barack Oboma. Kutokana na kitendo cha baadhi ya magari ya mawaziri wetu kunuswa na mbwa wa usalama. Ebo! kwani mawaziri sio wanasiasa! Mwigulu alishanadi kuwa baadhi ya wanasiasa wetu ni magaidi, tulitarajia nini? Hakika ni aibu. Niaibu kwasababu mwisho wa siku Lwakatare alionekana kuwa siyo gaidi nakwamba
ushahidi aliokuwa anautegemea kiasi cha kujiapiza kwa muumba ulikuwa ni feki. Mkanda wa video wa kuungaunga ambao bila shaka Mwigulu alishakuwa nao. Alipewa nanani na kwanini, haifahamiki hadi leo.
ushahidi aliokuwa anautegemea kiasi cha kujiapiza kwa muumba ulikuwa ni feki. Mkanda wa video wa kuungaunga ambao bila shaka Mwigulu alishakuwa nao. Alipewa nanani na kwanini, haifahamiki hadi leo.
Labda kupitia makala haya atatujibu watanzania. Nabado anatakiwa kutujibu anampango gani wa kulisafisha taifa letu kutokanana tuhuma za kupika. Tafadhali Mwigulu atujibu watanzania kabla ya kutaka tumpe urais wa nchi.

Wote mtakumbuka alivyoongoza kampeni katika uchaguzi mdogo wa Igunga kupitia CCM. Sarakasi za Mwigulu mnazikumbuka vema, licha ya chama chake kushinda, lakini aliacha maumivu makubwa kwa vijana wa kule na maeneo mengine ambapo baadhi ya vijana walisota ndani nakufunguliwa mashitaka ya bandia. Kama aliweza kutengeneza uongo mzito ndani ya bunge kiasi cha dunia kuamini, kwanini tusishuku na kuamini yaliyotokea Igunga wakati na baada ya uchaguzi ni mkakati wake kwa manufaa ya chama chake? Niyeye aliyemtembeza kijana aliyemwagiwa tindikali katika uchaguzi huo mithili ya mwenge wa uhuru. Lengo nikuonesha mfumo wa vyama vingi unamadhara.
Walengwa wakubwa ni CHADEMA. Shabaha yake kifutwe. Kwangu mimi kitendo kile ni chakikatili kwa yule kijana, kwa kumtembeza na kumdhalilisha kiasi kile. Alikosa utu na huruma kabisa. Kibaya zaidi hakuonywa akaachwa afanye alivyofanya eti kwa vile kulikuwa na maslahi ya chama chake. Kumbe kwa wapenda demokrasia walimuona ni janga la demokrasia.
Kwa menendo huu nirahisi kumlia dhambi hata kudhururiwa kwa kijana yule alihusika ilikufikia lengo. Kwanini alikosa huruma na kumfanya ni mtaji wakisiasa? Leo anataka tumpe urais wa nchi! Ndipo ninapowatahadharisha viongozi, wafuasi na wanachama wa vyama vya siasa vya upinzani.
Siku ya kuapishwa Mwigulu kuwa rais, basi someni dua kwa imani mnazofuata na kuziamini wakati shingozenu mumeeleza kibla mkisubiri kufyekwa kwa amri ya rais.
Wala tusimuamini na kuyaamini yale aliyokuwa anayaeleza kama vipaumbele vyake. Muongo! yale aliyoyaeleza ndiyo yalikuwa yanaelezwa na kulalamikiwa na kambi ya upinzani bungeni. Yeye ndiye aliyekuwa kinara wa kupinga huku akishangiliwa na kutuzwa fedha nawenzake wenye maono hafifu. Leo anaibuka nakuchukia uchunguzi juu ya uchunguzi, wamachinga na mama lishe kufukuzwa kama digidigi. Mwigulu we, mwogope Mungu! Nikweli uhenda aliishi maisha ya shida lakini alipopata madaraka hakuwakumbuka wenzake wanaopata shida. Badala yake waliojitokeza kuwatetea aliwabeza. Leo anakumbuka shuka aliyoitupa ili amalizie usingizi.Haiwezekani.
Wala tusimuamini na kuyaamini yale aliyokuwa anayaeleza kama vipaumbele vyake. Muongo! yale aliyoyaeleza ndiyo yalikuwa yanaelezwa na kulalamikiwa na kambi ya upinzani bungeni. Yeye ndiye aliyekuwa kinara wa kupinga huku akishangiliwa na kutuzwa fedha nawenzake wenye maono hafifu. Leo anaibuka nakuchukia uchunguzi juu ya uchunguzi, wamachinga na mama lishe kufukuzwa kama digidigi. Mwigulu we, mwogope Mungu! Nikweli uhenda aliishi maisha ya shida lakini alipopata madaraka hakuwakumbuka wenzake wanaopata shida. Badala yake waliojitokeza kuwatetea aliwabeza. Leo anakumbuka shuka aliyoitupa ili amalizie usingizi.Haiwezekani.
Mwigulu ameeleza mipango na mbinu za kusukuma uchumi nk. Lakini mbona chama chake nacho kinaishi kwa kuhemea wakati alishakuwa mtunza hazina wake na naibu katibu mkuu? Kwanini maarifa hayo asianze kuyapeleka kwenye chama ilikuondokana na utegemezi? Anatudanganya!
Yapo mambo lukuki kuhusiana na kijana huyu. Simchukii kwa kumuonea bali matendo yake ni ya hatari yatavuruga mshikamano wetu. Kama alizawadiwa vyeo kwa vitendo hivyo na kikundi au mtu ni bora abaki navyo hivyo na aishie hukohuko. Kuliko kututaka wananchi tumpe urais wetu atutie kwenye dhahama.
Yapo mambo lukuki kuhusiana na kijana huyu. Simchukii kwa kumuonea bali matendo yake ni ya hatari yatavuruga mshikamano wetu. Kama alizawadiwa vyeo kwa vitendo hivyo na kikundi au mtu ni bora abaki navyo hivyo na aishie hukohuko. Kuliko kututaka wananchi tumpe urais wetu atutie kwenye dhahama.
Mtu aachi tabia yake ya asili, kwakuwa anatabia ya kupenda sifa na kujipendekeza hataacha. Badala yake atajipendekeza kwa marais wa mataifa makubwa na kukubali kufanya kila atakalo ambiwa. Ikifikia hatua hiyo itakuwa ni janga kwetu. Tena atasababisha hata mataifa jirani na ya mbali yatutenge kutokana na vijineno anavyoweza kuvipeleka kwa viongozi wa mataifa makubwa ili aonekane ni bora kuliko viongozi wa mataifa mengine.
Watanzania wenzangu, nimuda wetu wakuwapima ili tuwahukumu kwa haki hawa wanaotangazania. Tusiwahukumu kwasababu ya vyama wanavyopitia bali vitendo vyao. Nasasa tufungue makabati tujikumbushe rekodi zao. Iwe mapema kabla ya kutangaza ili wanapotangaza tuweze kulinganisha.
Nimegundua kuwa watu wengi tumekuwa wasahaulifu sana. Nahiyo nihatari, tunaweza kuchezeshwa kishetani wakati nyimbo nizakimalaika. Nahii inatokana na wengi wetu kuacha na kushindwa kufauatilia siasa zetu na nje. Matokeo yake tunakosa rekodi za hawa watu. Tungekuwa tunautamaduni huo wala tusingehaika kabisa kumpata kiongozi sawia. Bali kwa mwenendo huu, Tanzania inaweza kuwa na kiongozi jambazi. Maana baadhi yetu ingawa tunajua kwamba hii ni nchi ya ujamaa, lakini ghafla tumegeuka na kuwashangalia mabepari na mafisadi na kutaka kuwapa nchi.
Wengine wanashikilia na kumshabikia mtu kwasababu ni mfurukutwa, mkereketwa, kada wachama chake na anayepigania maslahi ya chama badala ya wananchi na taifa. Tubadilike sasa natuanze kufuatilia na kushiriki siasa wakati wote badala ya kusubiri kipindi cha uchaguzi.
Nitaendelea na wengine panapo majaaliwa. Kaeni mkao wa wa kula. Haachwi mtu hapa.MUNGU IBARIKI TANZANIA. 0757115973/ 0717924695.
Tags
MAKALA