MKOA WA LINDI WAFANIKIWA KATIKA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA, IDADI KAMILI YA KIMKOA HII HAPA

Na Abdulaziz, Lindi
MKOA wa Lindi, umemaliza zoezi la uandikishaji kwa kuandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura, kwa kuvuka lengo la kuandikisha watu 509,224 waliokuwa na sifa watakaoshiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
BVR
Takwimu hizo zimetolewa na Afisa uandikishaji mkoani hapa, Mwinjuma Mkungu alipokuwa anazungumza na mwandishi wetu Ofisini kwake mjini Lindi.Mkungu amesema mkoa uliweka lengo la kuandikisha watu 494, 515, lakini waliojitokeza kuitumia Haki yao ya kujiandikisha ni, 509,224 sawa na asilimia 101% ya waliokadiliwa katika zoezi hilo, ambalo limechukuwa takribani mwezi mmoja.“Kwa upande wetu mkoa tuliweka lengo la kuandikisha watu walio na sifa wapatao 494,515,lakini waliojitokeza na kuweza kuandikishwa ni zaidi ya hao,na kufanya ongezeko la watu 14,709”Alisema Mkungu.Amefafanua kwa kusema Lindi vijijini, ndiyo inayoongoza kwa kuandikisha watu (109,041) wakati lengo lilikuwa (100,330), ikifuatiwa na Kilwa iliyoandikisha (106,512) huku makadirio yalikuwa (106,387), ambapo Nachingwea waliojitokeza na kuandikishwa ni (104,823), lengo lilikuwa ni (105,519).Ruangwa walioandikishwa ni (83,672) wakati lengo (82,795), Liwale (56,507) huku makadirio ni watu (51,947) na Lindi Manispaa ni ya mwisho kwa kuandikisha watu (48,850) lengo lilikuwa ni kuandikisha (47,356).Afisa uandikishaji huyo amesema mafanikio hayo yamechangiwa zaidi ni pamoja na vyama vya siasa kusimama kidete kutoa elimu ya uhamasishaji wananchi walio na sifa, umuhimu wa kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura ili muda utakapofika waitumie kuchagua viongozi wanaowataka.Mkungu amesema pamoja na kujitokeza kwa kasoro ndogondogo wakati wa zoezi la uandikishaji kwa baadhi ya maeneo, lakini yaliweza kurekebishwa na kuweza kukamilika kwa muda uliopangwa.Alizitaja baadhi ya changamoto ambazo zilijitokeza wakati wa zoezi hilo la uandikishaji ni pamoja na (BVR) kutofanyakazi kwa baadhi ya maeneo, ikiwemo kutosoma system na maopereta kutokuwa na spidi wakati wa kuandikisha.“Ukiondoa changamoto hizo,hakukuwa na matatizo mengine,kwa upande wetu kama mkoa tunashukuru mungu zoezi limekwenda kwa amani na muda uliopangwa”Alisema Mkungu.

Zoezi la uandikishaji watu katika Daftari la kudumu la wapiga kura, ndani ya mkoa wa Lindi, lilianza rasmi April 24 na kukamilika Mei 28 mwaka huu.
Previous Post Next Post