Wanawake nchini wametakiwa kujitokeza kuomba nafsi mbalimbali za uongozi sambamba na kuacha tabia ya kujengeana chuki badala yake waungane jitokeza kuomba nafsi hizo.
Ghasia alisema kuwa ili wanawake waweze kujikomboa na kutimiza azma ya asilimia 50 kwa 50 vyema kipindi hiki cha uchaguzi wakajitokeza kuomba nafsi za uongozi na kuwapigia kura wanawake waliodhubutu kufanya hivyo. Alisema kuwa mafanikio ya mambo hayo hayawezi kufikiwa kama wanawake nchi watatumiwa kwa wakutenganisha wazeo kwa kujengewa chuki ili wakose umoja na mshikamano.Aidha ghasia alizitaka halmashuri za wilaya nchi kutekeleza agizo la serikali kutenga fedha asilimia 10 kwa ajili ya kuvisaidia vikundi vya vijana na wanawake ili waweze kupambana na umaskini.Awali mkuu wa mkoa wa Lindi Mwatumu Mahiza alisema madhumuni ya semina hiyo ni kuwawezesha wanawake kupata ufahamu na uelewa wa nafsi yao katika jamii wajibu na haki zao.Mahiza aliongeza kuwa kufanikiwa kwa semina hiyo yametokana na utekelezaji wa agizo la serikali la kuzitaka halmashauri za wilaya wilaya mkoani humo kutenga asilimia 5 ya mapato ya ndani kugharamia ufuko wa maendeleo ya wanawake.
Tags
HABARI ZA KITAIFA