Na.Ahmad Mmow-Nachigwea.
Hatimaye waziri wa mambo ya ndani ya nchi na mbunge wa Nachingwea, Mathias Chikawe, amevunja ukimya na kutegua kitendawili cha muda mrefu. Baada ya JANA kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kugombea urais katika uchaguzi ujao. Chikawe ambaye ametangaza nia hiyo nyumbani kwake mjini Nachingwea mkoani Lindi.
Hatimaye waziri wa mambo ya ndani ya nchi na mbunge wa Nachingwea, Mathias Chikawe, amevunja ukimya na kutegua kitendawili cha muda mrefu. Baada ya JANA kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kugombea urais katika uchaguzi ujao. Chikawe ambaye ametangaza nia hiyo nyumbani kwake mjini Nachingwea mkoani Lindi.

Alisema tangu miaka minne na nusu iliyopita alianza kujitathimini ili kuona kama anaouwezo wa kuifanya kazi hiyo ambayo alikiri kuwa ni ngumu. Hivyo amebaini kuwa anatosha, anaiweza na kuitendea haki kwa maslahi mapana ya nchi iwapo atapewa ridhaa hiyo. Alisema kuanzia mwaka 1983 amefanya kazi ofisi ya rais ambapo alifanya kazi na marais wa awamu takribani zote, hivyo anaujua ugumu wa kazi hiyo. Hata hivyo kutokana na uzoefu alioupata anaamini anaiweza. "Nimeona uzito wa kazi ile, ni ngumu kiasi cha kusababisha wanaoingia wakiwa vijana wanazeeka ghafla kutokana na majukumu mazito kwani ndiyo wenye kufanya na kutoa maamuzi ya mwisho kwa maslahi ya nchi," alisema Chikawe. Chikawe akieleza kwani hakutangaza mapema kama watangaza nia wengi walivyofanya,nabadala yake alifanya kuwa ni siri. Alisema anajua kwamba watu wenye uamuzi ndani ya chama chake ya kumpitisha agombe au kutompitisha niwachache ambao wapo kwenye vikao mbalimbali vya maamuzi ndani ya chama. Kuanzia sekretaeti hadi mkutano mkuu wa taifa. Hivyo hakuona sababu ya kutangaza hilo kwa watu wote. Kwani siyo jambo la ajabu kwani hata baadhi ya marais waliotangulia hawatangaza kwa umma kwamba watatangazania.Kuhusu vipaumbele vyake pindi akichaguliwa kuwa rais.Alisema atavieleza, tarehe 10 mwezi huu atakapozungumza na wanahacri mara tu baada ya kuchukua fomu.Hata hivyo alisema kipaumbe chake kikubwa kitakuwa ni kupambana na rushwa na ufisadi.
Kwa kauli mbiu ya pambana na wachache kwa maslahi ya wengi. Alifafanua kuwa rushwa na ufisadi nitatizo kubwa lakini wanaotenda ni wachache, ikiwamo vikundi vya watu wachache ambao wamekuwa wakijitokeza kwenye kashifa nyingi za ufisadi na kijitokeza kwenye kila kashifa za ufisadi. Kuhusu kazi kubwa atayoifanya itakuwa nini pindi akichaguliwa na kuwa Rais. Chikawe alisema kazi kubwa ya serikali ni kuendesha nchi kwa kuhakikisha wananchi wake wanakuwa salama na nchi inakuwa na amani na utulivu wakati wote ili wananchi waweze kufanya kazi za maendeleo na kufanya utekelezaji wa ilani na sera za nchi kutekelezwa kwa ufanisi.Kazi ambayo alibainisha anaiweza kutokana na uzoefu alionao kwakuwepo muda mrefu serikalini na wizara anayoingoza."Nilipoingia kwenye wizara hii nilikuta mambo mengi ikiwa matukio ya mabomu na mengine mengi, nikawaambia wenzangu nikikisikia mabomu na tindikali tena, tutaondoka wote kwa hiyo kazi ya kuendesha utawala wa nchi na kuhakikisha usalama na utulivu nimeianza nanimeizoea,"alisema.
Alisema matunda ya kazi yake kwenye wizara hiyo ngumu ambayo imesababisha kuongozwa na mawaziri 23 tangu huru, na yeye kuwa waziri wa saba katika utawala wa rais Kikwete, yameonekana. Kwani matukio hayo na mengine ya kihalifu yamepungua kwa kiasi kikubwa na kusababisha utulivu mkubwa. Naye mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa wilaya ya Nachingwea, Albert Mnali. Alitoa wito kwa yeyote atakayebahatika kuchaguliwa kuwa rais kupitia chama hicho, aongeze kasi ya kuhakikisha chama kinarejeshwa mikononi mwa wakulima na wafanyakazi ili waweze kuwa nasauti nacho. Kwani sasa watu wenye fedha wanaelekea kukiteka na kuanza kuwa nasauti. Ingawa juhudi za kukemea hali hiyo zinafanywa na viongozi wa chama hicho waliomadarakani.
Tags
HABARI ZA KITAIFA