Na. Abdulaziz Ahmeid, Lindi.
Kuelekea uchaguzi mkuuu, unaotarajiwa kufanyika mwezi wa oktoba mwaka huu. Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) wilaya ya Lindi kwa kauli moja umepitisha azimio la kumuomba mke wa rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Salma Kikwete, aombe ridhaa ya CCM ili agombee ubunge katika jimbo la Lindi mjini. Azimio hilo lilipitishwa na viongozi wa jumuia hiyo wangazi za matawi, kata na wilaya waliokutana katika ukumbi wa Andrea Kagwa hapa Lindi. mwishoni mwa juma lililopita.
Salma Kikwete akihutubia wananchi wa lindi katika moja ya ziara zake mkoani hapa katika Uwanja wa Ilulu, (Picha kutoka maktaba)
Wanawake hao walisema ili jimbo hilo liweze kurudi mikononi mwa CCM, kutoka kwa mbunge wa sasa, Salum Barwany wa CUF. Walisema chama hicho hakinabudi kumsimamisha Salma kugombea, kwani ni mtu sahihi anayeweza kukipatia ushindi. Mwalimu Zuhura Mohamed, alisema Salma aombwe kugombea nafasi hiyo kwasababu anazosifa zinazoweza kukifanya chama hicho kupata ushindi kirahisi kwa madai kuwa anauzika.
Mwalimu Zuhura alisema ilikudhihirisha wanamuhitaji. Wajumbe wa mkutano huo wafanye harambe ya fedha ambazo atakabidhiwa mke huyo wa rais ili achulie fomu. Wazo la mwalimu Zuhura liliungwa mkono na wajumbe wote wa mkutano huo, na kuanza harambee iliyofanikisha kupatikana shilingi 312,000.00 ambazo atakabidhiwa mjumbe huyo wa halmashauri kuu ya taifa wakati anaombwa aridhie kuomba ridha ridhaa ya chama hicho aweze kugombea nafasi hiyo ya uwakilishi bungeni.
Awali akifungua mkutano huo uliokuwa na lengo la kupanga mikakati ya ushindi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu. Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lindi, Muhsin Ismail. Aliwataka viongozi hao kuondoa makundi yanayosabisha mpasuko ndani ya chama. Alisema sababu kubwa iliyosababisha jimbo hilo kuchukuliwa na mgombea wa chama cha upinzani katika uchaguzi mkuu uliopita ni makundi yaliyosababisha mpasuko. Ambao ulitumiwa vizuri na vyama vya upinzani na kusababisha baadhi ya wanachama wa chama hicho kumpigia kura mbunge wa sasa wa jimbo la Lindi mjini, Salum Barwany wa CUF.
Naye aliyepata kuwa afisa mwandamizi wa CHADEMA, Ali Chitanda. Aliwataka wanawake hao kuwa chagua wanachama waadilifu ili chama hicho kisiendelee kushambuliwa na ufisadi. "Msipo kuwa makini katika kuchagua mjue tuendelea kutukanwa hadi tukione chama ni kichungu, kumbe kosa kubwa ni aina ya watu tunawachagua kutoka kwenye chama chetu," alionya Chitanda.
Mkutano huo ulihudhuri wa nawajumbe 220 ambao ni viongozi wa umoja huo wa matawi na kata zilizopo katika wilaya hiyo.
Tags
HABARI ZA KITAIFA