PATA KUJUA JINA ALILOPEWA KITUKUU CHA MALKIA ELIZABETH WA UINGEREZA

Kitukuu wa Malkia ElizabethKitukuu wa Malkia ELIZABETH wa uingereza apewa jina

Hatimaye kitukuu cha Malkia ELIZABETH, wa UINGEREZA kilichozaliwa mwishoni mwa wiki iliyopita kimepata jina. Kitukuu hicho ambacho ni mtoto wa WILLIAM na KATE, mjukuu wa Malkia, kimepatia jina la CHARLOTE ELIZABETH DIANA.
Mtoto huyo wakifalme amepatiwa majina ya wanawake wa ukoo wa kifalme wa UINGEREZA, ambapo CHARLOTE, aliishi karne ya 18 na alijipatia umaarufu kwa kuzaa watoto wengi katika ukoo huo.

ELIZABETH ndiye malkia wa sasa na DIANA ni mama wa WILLIAM, aliyefariki dunia kwa ajali ya gari na alikuwa akipendwa sana na raia wengi wa UINGEREZA kutokana na tabia yake ya kupenda watoto na kuwa na huruma kwa wenye shida.

Sherehe za kupewa jina mtoto wa kifalme zimeambatana na taratibu za kifalme za kupigwa kwa mizinga nje ya jengo la kifalme.
Previous Post Next Post