Watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa wakati wakikabiliana na polisi katika eneo la mto kahabwe katika wilaya ya kakonko katika tukio ambalo polisi wamefanikiwa pia kukamata bunduki moja ya kivita, mabomu mawili na risasi 33.
Kamanda wa polisi mkoa wa kigoma Frednand Mtui amesema watu hao pamoja na wenzao ambao walifanikiwa kukimbia, walikutwa na polisi waliokuwa doria katika eneo hilo la mpaka kati ya wilaya ya kakonko na kibondo na kuanza kurushiana risasi zilizosababisha vifo vya majambazi hao ambao hawajatambulika hadi sasa.
Katika tukio jingine watoto wawili wa familia moja Rashid Juma (3), Mwajuma Juma( 1) wakazi wa kijiji cha chankabwimba wilayani kigoma, wamekufa baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kushika moto kufuatia dada yao mwenye umri wa miaka saba kuacha kibatari kikiwaka baada ya kujiandaa kwenda shule asubuhi ambapo chandarua kilishika moto na kuunguza nyumba yao.