MSHALE WA ILULU: MAGAMBA YANAANZA KUFUNIKA KICHWA.CCM WAVIVU WA KUCHAGUA ACHA WAULE WA CHUYA.

Na.Ahmad Mmow. LINDI
Imeandikwa: Imani bila matendo imekufa, kwamba kuwa na imani bila matendo yanayoendana na imani ya mja kwa kile anachoamini ni niswa na kutoamini kabisa ambacho mja anaamini.
wananchi wakisema no
Kwani imani pekee bila ya matendo hayawezi kumpa binadamu uzima wa milele.Wapo wanaohubiri kwamba usifuate matendo yangu bali maneno yangu. Hayo ni maneno ya baadhi ya viongozi wa dini ambao dhahiri maneno yao hayaendani na vitendo vyao.

Kwakuwa wanajua kuwa matendo yao yanajulikana na waumini wanaowaongoza, ndipo wanapokuja na kauli hiyo ya kinafiki. Wanajua kuwa wanatenda dhambi, lakini wanataka kuendelea kuaminiwa na binadamu. Hakika hawataokoka, watakumbana na hasira za muumba. Kwani imeandikwa kuwa malipo ya dhambi ni mauti. 

Nimetanguliza kueleza maneno hayo yaliyo kwenye aya za kitabu kitakatifu cha dini, baada ya kulinganisha na ya kuhubiri imani lakini ukichukua hatua(vitendo) ni dhahiri malipo ya dhambi hiyo ni mauti. Mauti ya chama nikusambaratika, ingawa siombei yatokee hayo.

Lakini kwa hali ilivyo nikudura ya MUNGU tu kinaweza kuwa salama. Vitabu vya Dini vinatuambia na kutupa imani kuwa kwake yeye hakuna linaloshindikana. Kwani kwa sisi binadamu ni rahisi kusema haiwezekani, lakini kwa MUNGU inawezekana. Yote kwa yote itakavyokuwa niukweli usiopingika kwamba chama hicho kinawakati mgumu na kinapita katika wakati mgumu.

Walioitwa magamba wanaelekea kukizidi nguvu, nakwahakika nguvu zao zinakilemea chama hicho. Kuwaondoa sasa ni maafa na kuwaacha wafikie na kufanikiwa wanachotaka ni janga. Malipo ya dhambi ni mauti. Chama kipo kwenye mtanziko mithili ya kenge mla mayai aliyemeza mayai yaliyochemshwa. Kenge huyo anakuwa katika mateso makubwa, kwani ningumu kwake kutema mayai hayo kama ilivyo ngumu kuyameza. Taratibu anaweza kufa. Malipo ya dhambi ni mauti! 

Binafsi nasubiri kwa hamu nijinsi gani chama hicho kitakavyowanadi wale walioitwa magamba pindi wakiwa wagombea wa chama hicho na kufanikiwa kukipa ushindi katika uchaguzi ujao. Kwa upande mwingine nasubiri kwa hamu jinsi watakavyojichuna magamba hayo yaliyogeuka ngozi imara na kukiacha kikiwa salama.

Ugumu wote huo unatokana na kuhubiri imani ambayo haikuwa na matendo. Wahenga walishatuambia kwamba mchelea mwana kulia hulia mwenyewe, tena mvivu wa kuchagua hula wa chuya. Ebu tusubiri tuone ufundi utakaofanywa na chama hicho kikongwe ili kivuke salama kihunzi hicho.

Bali kama magamba yenyewe yalifananishwa na mdudu nyoka, basi ipo hatari kubwa kama watalazimisha kuchuna. Kwani nyoka hawezi kuishi na jereha, nyoka haimili kidonda. Lazima atakufa, labda iwe gamba la mti. Hata hivyo mti hauna gamba bali gome. Bila shaka gamba hilo nila nyoka. Basi natusubiri ufundi na maajabu ya karne.
Previous Post Next Post