PICHA:: HIVI NDIVYO MH. LOWASA ALIVYOANZA "SAFARI YA MATUMAINI" MJINI ARUSHA

Edward Lowassa
Gari iliyombeba Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa ikipita nje ya uwanja wa Sheih Amri Abeid, jijini Arusha mapema leo asubuhi wakati akielekea kwenye Ofisi za CCM Mkoa. Mh. Lowassa anatarajia kulihutubia taifa mchana wa leo kwenye uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid, ikiwa ni sehmu ya kutangaza kwake nia yake ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Edward Lowassa
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuwepo kwenye ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha.Kulia ni Mkewe Mama Regina Lowassa.
Edward Lowassa
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole.
Edward Lowassa
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa alieambatana na Mkewe, Mama Regina Lowassa pamoja na wanaCCM wengine.
Edward Lowassa
Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole (hayupo pichani).
Edward Lowassa
Mh. Edward Lowassa katika picha ya Pamoja na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole

(Picha zote kwa hisani ya Othman Michuzi)

ENDELEA KUWA NASI KWA PICHA ZAIDI ZA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID ZITAWAJIA BAADAE KIDOGO
Previous Post Next Post