Unknown Unknown Author
Title: SERIKALI YACHOMOZA MAKUCHA YAKE KWA WAWEKEZAJI WA KICHINA, WAFUNGA MGODI WA SUN SHINE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Serikali imeufungia mgodi wa SUN SHINE unaomilikiwa na wawekezaji wa kichina katika kijiji cha MATUNDASI wilayani Chunya kuendelea na uch...
Kiwanda
Serikali imeufungia mgodi wa SUN SHINE unaomilikiwa na wawekezaji wa kichina katika kijiji cha MATUNDASI wilayani Chunya kuendelea na uchimbaji wa dhahabu kutokana na mgodi huo kuharibu mazingira kwa kiwango cha juu, huku pia ukiendesha shughuli zake katika mazingira machafu yanayohatarisha afya za wafanyakazi na wananchi wanaoishi kuzunguka mgodi huo.

Baraza la usimamizi wa mazingira NEMC ndilo ambalo limeufungia mgodi huo mpaka pale uongozi wake utakapotekeleza maelekezo ambayo yametolewa ya kuhakikisha wanaweka miundombinu ya kuhifadhi maji yanayozalishwa na mgodi, ambayo tayari yamesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira sambamba na kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa mgodi huo.

Meneja msaidizi wa mgodi wa SUN SHINE, Endy Wu amekiri kupokea na kusimamisha shughuli za mgodi huo na kuahidi kutekeleza maelekezo yote ambayo yametolewa na NEMC.

Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo,wamekiri kuanya kazi katika mazingira magumu, huku wakikabiliwa na matatizo lukuki, lakini wakaiomba serikali kuwasaidia kupata haki zao katika kipindi hiki ambacho mgodi huo umefungiwa.

Mkuu wa wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro amesema kuwa serikali ya wilaya yake itasimamia ili kuhakikisha yale yote ambayo yameagizwa na NEMC yanatekelezwa.

About Author

Advertisement

 
Top