Unknown Unknown Author
Title: DK SLAA AKOSOA MFUMO WA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KWA KUTUMIA MFUMO WA BVR
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Katibu mkuu chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa, ameendelea kukosoa mfumo wa uandikishaji wa daftari la kudumu l...
Dr.Slaa
Katibu mkuu chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa, ameendelea kukosoa mfumo wa uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mashine za BVR kuwa mfumo huo hauajwahi kuoinyesha tija kwa nchi yenye miundombinu bora kama Marekani.

Akihojiwa na vyombo vya mbalimbali vya habari kwenye uwanja wa Ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar-es-Salaam, mara baada ya kuwasili kutoka nchini marekani kwenye ziara ya kikazi ya siku kumi, Dkt Slaa amesema licha ya mchakato wa uingizaji mashine hizo kugubikwa na utata, mfumo huo haujawahi kuonyesha tija kwa nchi kama marekani na kuwa hiyo ni njia ya kuvuruga zoezi la upigaji kura na matokeo ya uchaguzi.

Aidhaa Dkt Slaa amepinga muswaada wa sheria ya mitandao ya kijamii na kuitaka serikali kuacha kubana uhuru wa habari nchini kwa kuweka sheria kandamizi kwa wananchi kutoa na kupokea taarifa kwani mitandao hiyo imechangia wananchi wengi kupata elimu na kuwa atakuwa wa kwanza kufungwa mara matumizi ya sheria hiyo yatakapo anza na kuwa haita dumu kwa mwaka 2016.

Katibu mkuu huyo ameendelea kumuomba Ras Jakaya Kikwete kuicha nchi kwenye mikono salama kwa kuhakikisha kuwa haongezi muda wa utawala wake na kudai kuwa nchi nyingi zilizoingia kwenye machafuko chanzo ni serikali iliyomadarakani kukiuka taratibu kwa kuvunja katiba.

About Author

Advertisement

 
Top