Unknown Unknown Author
Title: ALIYEKUWA RAIS WA MISRI AHUKUMIWA MIAKA 20 JELA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MOHAMED MORSI Mahakama nchini MISRI imemhukumu miaka ISHIRINI jela aliyekuwa rais wa nchi hiyo MOHAMED MORSI kwa kosa la kuwachochea wafu...
Mohamed MorssiMOHAMED MORSI

Mahakama nchini MISRI imemhukumu miaka ISHIRINI jela aliyekuwa rais wa nchi hiyo MOHAMED MORSI kwa kosa la kuwachochea wafuasi wake kumuuwa mwandishi wa habari na waandamanaji wa upinzaji katika makabiliano nje ya IKULU ya rais mwaka 2012.

MORSI aliyeondolewa madarakani na jeshi mwaka 2013 alikuwa anashitakiwa pamoja na wafuasi wengine wa chama cha MUSLIM BROTHERHOOD.
Hii ni mara kwanza kwa rais aliyechaguliwa kidemokrasia kuhukumiwa kifungo jela nchini humo. Awali mawakili wanaomtetea MORSI walisema agekabiliwa na hukumu ya kifo.

Mamia ya wafuasi wa kundi la MUSLIM BROTHER HOOD wamehukumiwa kifo katika mikakati ya kukabiliana na kundi hilo lililopigwa marufuku na rais wa sasa ABDUL FATAH AL SISI.

Kundi la MUSLIM BORTHER HOOD limemlaumu rais kwa kutumia mamlaka kama silaha.

About Author

Advertisement

 
Top