Unknown Unknown Author
Title: NHIF NA PSPF WATOA ELIMU KWENYE MKUTANO MKUU WA VIONGOZI WA CWT MKOA WA LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Fortunata Raymond akitoa elimu kuhusu maboresho yanayoendelea kufanywa na mfuko mbele ya vi...
NHIF LINDI
Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Fortunata Raymond akitoa elimu kuhusu maboresho yanayoendelea kufanywa na mfuko mbele ya viongozi na wawakilishi wa chama cha walimu mkoa wa Lindi,wakati wa mkutano wa mwaka wa chama hicho,ambapo alisema kwa sasa katika kukabiliana na changamoto ya huduma ya dawa mfuko umeanzisha mkopo wa dawa na vitendanishi kwa vituo vilivyosajiliwa na mfuko, ambapo bodi ya wakurugenzi iliridhia kutolewa kwa mikopo hiyo tangu mwezi Oktoba.2014. Mkutano huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Chamikumbi mkoani hapa.
NHIF LINDI
Wajumbe wa mkutano wa mkuu wa chama cha waalimu mkoa wa Lindi wakimsikiliza meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya (hayupo pichani) Fortunata Raymond wakati akifafanua mikakati mbalimbali inayotekelezwa na mfuko katika kuhakikisha wanachama wa mfuko wanapata huduma stahiki na bora zaidi.
NHIF LINDI
Fabiani Erioh mwakilishi wa shule za msingi Lindi vijijini kwenye mkutano mkuu wa viongozi wa CWT, akitoa hoja baada ya mada zilizowasilishwa kutoka kwa mwezeshaji wa mfuko wa Taifa wa Bima ya afya.
NHIF LINDI
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Lindi Ramadhan Mtumwa akifafanua mafao yanayotolewa na mfuko huo mbele ya viongozi wa CWT mkoani hapa,ambapo alibainisha ubora mafao hayo kama vile fao Elimu,fao la uzazi,mikopo ya nyumba sanjari na mkopo wa kuanza maisha pale mwanachama wa mfuko anapopata ajira,hivyo alitoa wito kwa wanachama kuiona kuwa ni fursa.
NHIF LINDI
Kutoka kulia ni meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya Fortunata Raymond akichukua dondoo za hoja kutoka kwa wanachama wa mfuko,kushoto ni meneja wa PSPF Ramadhan Mtumwa mkoani Lindi akifuatilia kwa karibu.

About Author

Advertisement

 
Top