Unknown Unknown Author
Title: JK AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MKUU WA WILAYA YA KYERWA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rais KIKWETE aongoza waombolezaji kuaga mwili wa Mkuu wa wilaya ya KYERWA Rais JAKAYA KIKWETE ameongoza mamia ya wananchi jijini DSM ku...
Jakaya M kikwete
Rais KIKWETE aongoza waombolezaji kuaga mwili wa Mkuu wa wilaya ya KYERWA

Rais JAKAYA KIKWETE ameongoza mamia ya wananchi jijini DSM kuuaga mwili wa Mkuu wa wilaya ya KYERWA mkoani KAGERA Luteni Kanali Mstaafu BENEDICT KITENGA aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa ya MUHIMBILI jijini DSM kutokana na shinikizo la damu.

Miongoni mwa viongozi walioshiriki kuuaga mwili wa Marehemu KITENGA katika Hospitali ya Jeshi ya LUGALO jijini DSM ni Waziri Mkuu MIZENGO PINDA, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt HUSSEIN MWINYI na makamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa TANZANIA - JWTZ.

Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Kijiji cha KOLLA Mkoani MOROGORO kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho kutwa siku ya Alhamisi.

Mkuu wa Mkoa wa KAGERA JOHN MONGELLA amemwelezea marehemu KITENGA kuwa alikuwa ni mchapakazi na kiongozi shupavu ambaye muda wake mwingi aliutumia kuwashauri vijana maadili mema ya kazi.

Luteni Kanali Mstaafu BENEDICT alizaliwa mwaka 1953 mkoani MOROGORO na kushika nyadhifa mbalimbali za utumishi jeshini hadi alipostaafu mwaka 2008.

About Author

Advertisement

 
Top