Yanga walitangulia na kuongoza kwa Bao 2-0 zilizofungwa na Salum Telela na Haruna Niyonzima na FC Platinum kupata Bao lao Dakika za Majeruhi za Kipindi cha Kwanza.
Hadi Mapunziko Bao zilikuwa Yanga 2 FC Platinum 1.
Kipindi cha Pili Yanga walipiga Bao nyingine zaidi kupitia Amisi Tambwe na Mrisho Ngassa kupiga Bao 2 huku la 5 likitokana msaada mkubwa wa Mchezaji wa Liberia Kpah Sean Sherman alieingizwa kuchukua nafasi ya Simon Msuva.
Hadi Mechi kwisha Yanga 5 FC Platinum 1.
Timu hizi zitarudiana huko Zimbabwe Wiki mbili zijazo.
Yanga wametinga Raundi hii kwa kuitoa BDF XI ya Botswana kwa Jumla ya Mabao 3-2 na FC Platinum kuibwaga Sofapaka ya Kenya kwa idadi hiyo hiyo ya Magoli.
MATUKIO KAKIKA PICHA:
Simon Msuva akijaribu kuwatoka wachezaji wa Platnum Fc waliokuwa wamemzunguka kumzuia asilete madhara katika lango lao....
Mrisho Halfan Ngasa akiwatoka Mabeki wa Platnum katika Mechi ya Shirikisho iliyofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini dar es salaam Hivi leo na Yanga kuibuka washindi kwa bao 5 - 1.
Hamisi Tambwe akiwania Mpira wa Kichwa sambamba na Beki wa Platnum Fc ya zimbabwe katika Mchezo wa Shirikisho uliochezwa hivi leo jijini dar es salaam na Yanga kuibuka kidedea kwa goli 5 - 1, huku Hamisi tambwe akiwa miongoni mwa wafungaji hao.
Haruna Niyonzima akishangilia mara baada ya kuifungia timu yake ya Yanga bao la pili katika mechi ya Shirikisho iliyochezwa hivi leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Yanga imeshinda 5 -1.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.