Onesmo Olengurumwa Mratibu wa Kitaifa wa THRD-COALITION akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa Habari wa Mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi yanayofanyika katika Ukumbi wa Veta - Mtwara hadi tarehe 6/3/2015, Kuhusiana na Usalama na Tathmini ya Athari kwa waandishi wa Habari.
Waandishi wa habari wametakiwa kufichua vitendo vya ukiakaji wa haki za binadamu na kuwatetea wanyonge kwa kupaza sauti kwenye vyombo vya habari. Wito huo umetolewa leo na mkurugenzi wa mtandao wa ulinzi wa watetezi wa haki za binadamu(THRD), Onesmo Olengurumwa, alipozungumza na waandishi wa habari kwenye mafunzo ya waandishi wa habari wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma yanayofanyika mjini Mtwara.
Olengurumwa alisema kundi kubwa la wananchi wanyonge halina eneo linalotegemea sauti yake kupazwa na kusikika, zaidi ya waandishi habari kupitia vyombo vya habari. Alisema serikali inavyombo vyake vya kuisemea na kuitetea lakini wananchi ambao wengi wao ni wanyonge, hivyo kalamu za waandishi ni tumaini lao katika kuwatetea.
Aidha Olengurumwa aliwakumbusha waandishi hao kuandika habari bila upendeleo na kwakuzingatia uandishi wa amani badala ya uchochezi. "katika kuandika nivizuri mchukue tahadhari na kuweni waangalifu, tendeni haki pateni taarifa za kila eneo kuhusiana na habari husika bila kuegemea upande mmoja," alisema Olengurumwa.
Mkurugenzi huyo aliongoza kusema uandishi wa amani na unaozingatia haki utawafanya waaminiwe na jamii na hata vyombo vyenye mamlaka kiutawala ili kuepuka kuitwa wachochezi na majina mengine yasiyofaa,hasa wakati wa kupiga kura za maoni kwa katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu ujao.
"mwaka huu unahekaheka nyinyi ambazo siyo salama sana kwa waandishi na watetezi wa haki za binadamu,kuweni waangalifu kwani kuna suala la kura za maoni na uchaguzi mkuu," alionywa Olengurumwa.
Mafunzo hayo ya siku tatu kwa baadhi ya waandishi wa habari mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma yameanza leo katika mji wa manispaa ya Mtwara yanatarajiwa kumalizika tarehe 6 mwezi huu.
Mwanja Ibadi mwandishi wa gazeti la Mwananchi akiwa sambamba na John Mganga Mwandishi wa ITV wote kutoka Lindi wakiwa katika Mafunzo yalioanza leo hii katika Ukumbi wa Veta - Mtwara yanayotolewa na THRD-COALITION kuhusu Usalama na Tathmini ya Athari kwa Waandishi wa Habari
Waandishi wa habari wa Mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Veta - Mtwara katika Mafunzo ya Usalama na Tathmini ya Athari kwa Waandishi wa Habari Kuanzia Tarehe 4 - 6, 2015
Fungwa Kilozo kutoka Blog ya Lindi yetu akiwa sambamba na Joseph Mwambije Mwandishi wa ITV - Ruvuma katika Mafunzo ya Usalama na Tathmini ya Athari kwa Waandishi wa Habari yanayofanyika katika Ukumbi wa Veta Mtwara yalioanza Leo hii na yatadumu kwa siku Tatu.
Sijawa Omari Mweka Hazina wa Press Club Mtwara akiwa sambamba na Andrew Kuchonjoma Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club wakisikiliza mada zilizokuwa zikiendelea katika mafunzo yalioanza leo hii ya Waandishi wa habari wa Mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi yanayotolewa na THRD-COALITION katika ukumbi wa Veta - Mtwara
Juma Nyumayo (asiie na tai) akisikiliza mada zilizokuwa zikiendelea katika mafunzo yalioanza leo hii ya Waandishi wa habari wa Mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi yanayotolewa na THRD-COALITION katika ukumbi wa Veta - Mtwara
Abdulaziz Ahmeid Mwandishi wa Channel ten ambaye pia ni Mwenyekiti wa Press Club Lindi akiwa sambamba na Blogger wa Lindiyetu.com katika Mafunzo hayo yanayoendelea katika Ukumbi wa Veta - Mtwara.
Onesmo Olengurumwa Mratibu wa Kitaifa wa THRD-COALITION akitoa mada katika Mafunzo yanayoendelea katika Ukumbi wa Veta - Mtwara kuhusiana na Usalama na Tathimini ya athari kwa waandishi wa Habari yalioanza leo tarehe 4 - 6/3/2015
Waandishi wa Habari wa Ruvuma Mtwara na Lindi wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mratibu wa Kitaifa wa chama cha THRD-COALITION.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.