Unknown Unknown Author
Title: NDANDA FC YAICHAPA MARKET PLACE 2 - 1, MECHI YA KIRAFIKI UWANJA WA ILULU, LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha leo cha NDANDA FC kilichoanza Dhidi ya Market Place FC katika uwanja wa ILULU leo hii katika mchezo wa kirafiki.   Kikosi...
Ndanda FC
Kikosi cha leo cha NDANDA FC kilichoanza Dhidi ya Market Place FC katika uwanja wa ILULU leo hii katika mchezo wa kirafiki. 
Market Place FC
Kikosi cha leo Cha Market Place kilichoanza Dhidi ya NDANDA FC katika uwanja wa ILULU leo hii katika mchezo wa kirafiki. 

Na. Mwandishi Wetu, Lindi
Timu ya Ndanda Fc kutoka Mtwara inayoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania leo hii imecheza Mechi ya Kujipima nguvu na Mabingwa wapya wa Mkoa wa Lindi Timu ya Market Place yenye maskani yake Manispaa ya Lindi katika Uwanja wa Ilulu.

Mechi hiyo iliyoanza Majira ya Saa kumi na Dakika Ishirini na Tano Jioni ilihudhuriwa na Mashabiki Lukuki wa Manispaa za Lindi na Mtwara.

Timu ya Ndanda Fc ndiyo ilikuwa yakwanza kufanikiwa kufungua Kalamu ya Magoli katika Uwanja huo wa Ilulu kupitia Mchezaji wake Mahiri Omega Same ambaye aliweza kufunga kwa ustadi goli hilo kwa kuachia shuti kali kutoka nje ya eneo la Maguu Kumi na Mbili na kumuacha Mlinda mlango wa Marketi Place kushindwa kuokoa hatari hiyo na Kuiandikiia Timu hiyo Goli la Kwanza.
Market Place FC
Baada ya Goli hilo Ilionesha Dhahiri Timu ya Market Place walionekana kuingiwa na Hofu kwani walikuwa wakipoteza mipira mingi na nafasi za Kufunga, Nakuisaidia Timu ya Ndanda kupata Goli la Pili kupitia Mchezaji wake Saidi Issa na Matokeo hayo Kusomeka 2 - 0 Hadi kipindi cha Kwanza kinaisha.
Ndanda FC
Kipindi Cha Pili Waalimu wote wa Timu zote mbili waliweza kufanya marekebisho katika Timu zao na Kuweza kuwaingiza wachezaji wengine wa akiba na Ilikuwa nifaida kwa Timu ya Market Fc kwani walionekana kucheza kwa Kutulia sana na Kuweza kupata Goli maridadi la kufuta machozi kupitia Mchezaji wake Mohamed Bilal.

Hadi mwisho wa Mchezo huo Marketi Fc 1 - Ndanda Fc 2

Ngawina Ngawina
Aidha Kocha Msaidizi wa Ndanda FC Ngawina Ngawina, aliweza kusema mechi hiyo ilikuwa muhimu kwao kwani wamepata fursa ya kufanya Majaribio kabla ya Mchezo wao wa Ligi kuu ya Vodacom hivyo mchezo huo utawajenga wachezaji wake na ameshaona mapungufu yaliyopo na ameahidi kuyafanyia kazi, pia amewasihi mashabiki kuisapoti timu hiyo ili iweze kufika mbali.
Kipanya Malapa
Nae Kocha wa market Fc Kipanya Malapa, amewapongeza Wachezaji wake kuwa wamecheza vizuri sana hasa kipindi cha pili kwani anajua kipindi cha kwanza walicheza kwa hofu kutokana na timu hiyo kuwa ni ya Ligi kuu, lakini waliweza kuzoea mchezo na kuweza kufanya vizuri hadi kupata goli moja la kufutia machozi, Pia amesema yakua wacchezaji wengi waliocheza leo ni wageni na hawaja weza kufanya mazoezi ya pamoja kwa muda mrefu hivyo anaamini wataweza fanya vizuri siku za usoni.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top