Baada ya Kura Kutotosha 2010 Abdulaziz Afungua Milango kwa wagombea Ubunge CCM Jimbo la Lindi Mjini
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini 2015 ambae pia ni mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Lindi Abdulaziz Ahmeid akiwa katika Picha ya Pamoja na Balozi wa Finland Nchini Bi Sinikka Antila
Na Ahmaid MMOW-Lindi
Kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu,Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel ten, Abdulaziz Ahmed Leo Ametangaza nia yake ya kugombea ubunge katika jimbo la Lindi mjini katika uchaguzi mkuu ujao kupitia Chama
cha Mapinduzi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Abdulaziz ambae pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Lindi alisema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kujitathimini na kugundua kuwa anao uwezo wa kuzikabili na kuzitafutia majibu yakinifu changamoto mbalimbali ziliopo katika jimbo la Lindi ambalo kwa sasa lipo chini ya Mbunge
toka CUF, Salum Barwany 'mwaka 2010 nliomba ridhaa ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi hata hivyo kura hazikutosha kupitia chama change na Jimbo kuchukuliwa na Upinzani na nimeona changamoto nyingi zimeendelea kuwepo kwa miaka nenda rudi bila kutafutiwa ufumbuzi wa uhakika Nipeni Ridhaa wana lindi niwatumikie kuliko ilivyotokea katika matarajio yenu 2010-2015'
Aidha alibainisha changamoto hizo ni pamoja na miundo mbinu ya barabara, maji, huduma za afya na umeme usio na uhakika huku Akiainisha kuwa nguvu na uwezo wake kushinda katika kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi na uchaguzi mkuu zipo mikononi mwa wananchi wa jimbo hilo na ambao wanakiu ya maendeleo na mabadiliko.
"sitegemei kutumia Fedha ili kuwa nunua wapiga kura bali wale wapenda maendeleo na mabadiliko ndiyo mtaji na silaha yangu, rushwa hapana kwani chama chetu hakitaki kabisa kitendo hicho kwa kuwa kinaathiri Maendeleo na kinaua chama cha Mapinduzi kwa Uwepo wa Makundi yanayotaka kupona maisha yao tu si maendeleo".
Katika uchaguzi mkuu uliopita Abdulaziz aliomba ridhaa ya chama chake cha mapinduzi lakini kwa mujibu wa kanuni na taratibu za CCM Kupitia kura za Maoni kumteua mgombea Bw Mohamed Abdulaziz ambae ni baba mdogo wa mgombea alichaguliwa kutetea chama hicho na kuangushwa na Salum Barwany katika Uchaguzi mkuu Lakini Wananchi watakuwa wamemtathimini nawatafanya uamuzi sahihi wa kumchagua.
Aidha alitoa wito kwa Vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha huku wengine wakijiunga na Chama hicho ili kumpigia kura Mgombea ambae anatoka katika kundi la Vijana kwa kuwa Vijana ndio Taifa La LEO
Sambamba na hilo Abdulaziz aliziasa kamati za chama na vikao vya uteuzi kuzingatia matakwa na maamuzi ya wanachama huku ikimea matumizi ya fedha kwa wagombea kuhonga wanachama ili wawapigie Kura
"Mpango huu wa kuhonga wanachama una athari kubwa kwa Chama Pia upo uwezekano wa kupata mgombea asiekubalika na kuendelea kutwaliwa na Upinzani ni lazima tuwe makini katika Ili Nina Imani hata Vijana toka vyama vya Upinzani wataniunga mkono na kunichagua kuwawakilisha," Alimalizia Abdulaziz alipokutana na waandishi wa habari
wa Vyombo Mbali mbali
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.