Unknown Unknown Author
Title: LIGI YA UINGEREZA :: MANCHESTER UNITED YAIFUNGA TOTTENHAM, LIVERPOOL NA SWANSEA KUSHUKA DIMBANI LEO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kocha wa Machester United Louis van Gaal amesema kuwa ushindi wa mabao matatu iliyoupata timu yake dhidi ya Tottenham ni jambo kubwa na a...
Kocha wa Machester United Louis van Gaal amesema kuwa ushindi wa mabao matatu iliyoupata timu yake dhidi ya Tottenham ni jambo kubwa na akasema walipaswa kushinda baada ya kutupwa nje ya FA Cup na wapinzani wao wakubwa Arsenal.
Goli la Marouane Fellaini, Michael Carrick na Wayne Rooney yalitosha kabisa kuwapa Mashetani wekundu pointi tatu muhimu na kuendelea kujikita katika nne bora ya msimamo wa ligi. Chelsea bado wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 64, huku Manchester City wakishika nafasi ya pili kwa pointi 58, washika bunduki Arsenal nafasi ya tatu kwa jumla ya pointi 57 huku nafasi ya nne ikiwa mikononi mwa Manchester United na pointi zao 56 kibindoni.
Rooney alishangilia kwa kucheza Ngumi na kisha kujidondosha chini akivunga amepigwa Ngumi na kuzirai ikiwa ni jibu la habari zilizozagaa mitandaoni hii Leo kuwa alipigwa Ngumi na kuzirai Jikoni Nyumbani kwake wakati akifanya mzaha wa kucheza Ngumi na Mchezaji wa zamani wa Man United Phil Bardsley ambae sasa anacheza Stoke City.

VIKOSI: MAN UNITED: De Gea, Vakencia, Jones, Smalling, Blind, Herrera, Carrick, Mata, Fellaini, Young, Rooney
Akiba: Lindegaard, Rafael, Blackett, Pereira, Januzaj, Falcao, Wilson

TOTTENHAM: Lloris, Walker, Dier, Vertonghen, Rose, Bentaleb, Mason, Townsend, Eriksen, Chadli, Kane
Akiba: Chiriches, Paulinho, Adebayor, Lamela, Vorm, Dembele, Davies

REFA: Mark Clattenburg

Huko Goodison Park, Wenyeji Everton waliichapa Newcastle Bao 3-0 kwa Bao za Dakika ya 20 za John McCarthy, Penati ya Romelu Lukaku ya Dakika ya 56 na la 3 kwenye Dakika za Majeruhi kupitia Ross Barkley.
Romelu Lukaku
Newcastle walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada ya Beki wao Fabricio Coloccini kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 59.
Ross Barkley

Ligi hiyo itaendelea tena leo ambapo Liverpool itakuwa ugenini kukabiliana na Swansea.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top