KUELEKEA UCHAGUZI 2015:: BABA KUNDAMBANDA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MASASI MJINI

Ismail Mapembe Kundambanda
Hatimaye msanii maarufu wa vichekesho na nyimbo ambae ni kipenzi cha watu wote na mkombozi wa wana wa kusini Ismail Mapembe maarufu Baba Kundambanda amechukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Masasi Mjini ndani ya Chama cha Wananchi CUF.

Akizungumza maneno hayo kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika Nyangao alitoa salamu kwa wana CCM kuwa yuko tayari kuwakomboa wana masasi na tayari ameshachukuwa fomu. 

Aidha vilevile alitambulisha nyimbo yake mpya ambayo ametaja ufisadi unaofanyika katika hospitali ya Nyangao na kuwataja majina mafisadi hao. Vilevile inasemakana Masasi Hakutoshi kutokana na aliyekuwa Mbunge kupitia tiketi ya CCM baada ya kusikia kuwa Baba Kundambanda kachukua fomu yeye ameghairi kugombea tena jimbo hilo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post