
Tukio hilo limetokea jioni hii mbele ya bustani ya Botanical kwa upande unaotazamana na geti kuu la kuingia Hospitali ya Ocean Road, baada ya kumkwapulia simu mwanadada mmoja (jina kapuni) aliekuwa akitembea kwa miguu na kwa bahati nzuri kulitokea msamalia aliekuwa na gari yake akaliona tukio zina na hapo ndipo alianza kuwafukuzia na mwisho wa mbio hizo ndio ukafika hapa baada ya kuzidiwa maarifa na pikipiki yao, hali iliyowapelekea kuanguka eneo hilo. Vijana hao walikamatwa na pikipiki yao ikachomwa moto.



Mdau akijipatia Selfie mbele ya pikipiki iliyokuwa ikiteketea kwa moto wakati huo.
Tags
HABARI ZA KITAIFA