PENINA KUPIGWA NDOA MUDA WOWOTE

MUIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Jennifer Raymond ‘Penina’, amefunguka kuwa anatarajia kufunga ndoa muda wowote kuanzia sasa.
 Jennifer Raymond ‘Penina’
Muigizaji wa filamu za Kibongo, Jennifer Raymond ‘Penina’.

Akizungumza na Uwazi, Penina alisema kuwa harakati za kuolewa zipo jikoni hivyo anamuomba Mungu kile ambacho kinatarajia kufanyika kiweze kwenda kama alivyopanga ingawa hakutaka kumweka wazi mwanaume huyo kwa madai kuwa hataki kuibiwa.
“Mambo ya ndoa yapo tayari na anayesubiriwa ni mwanaume ambaye anataka kunioa ili alete barua ya uchumba, kwa sasa yuko nje kwa ajili ya mambo yake binafsi lakini atakapotua tu Bongo, muda wowote ndoa itafungwa,” alisema.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post