Unknown Unknown Author
Title: MBUNGE WA CCM AMDAI JOYCE KIRIA TSH MILIONI 500
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria. MTANGAZAJI  wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amepokea samansi ya mash...
Joyce Kiria
Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria.

MTANGAZAJI wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria amepokea samansi ya mashtaka kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir (CCM) ambaye amedai amlipe fidia ya kumdhalilisha sh. Milioni 500 au amuombe radhi kupitia  kipindi chake.
Akiongea, Joyce Kiria alisema kuwa amepokea barua hiyo kwa mikono miwili na anawasubiri wanasheria wake ili waijadili.“Nilimpokea mke wa Mbunge aitwaye Hawa kama mwanamke mwenye matatizo ambaye alifika kutoa sauti yake ili watu wamsaidie mtoto wake mwenye ulemavu.
Baada ya kuongea naye nilimtafuta mheshimiwa ili kumpa nafasi naye aongee ya kwake kama wajibu wangu, lakini cha kushangaza yeye alinikamata na kunipeleka polisi, leo anasema nimemdhalilisha,” alisema Joyce .
Joyce anadaiwa fidia na Mbunge huyo kwa kuitangaza habari ya kumtelekeza mtoto mlemavu ambaye alilepelekwa kwenye kipindi chake na mkewe, Hawa Deusi.    

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top