Unknown Unknown Author
Title: MADSON FC YAIKACHA MARKET PLACE FC, LIGI DARAJA LA TATU - LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KIKOSI KIZIMA NA BENCHI LA UFUNDI LA MARKETI FC WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA TU YA MCHEZO WAO DHIDI YA MADSON KUTOCHEZWA LEO HII....
Madson Fc Vs Market FC
KIKOSI KIZIMA NA BENCHI LA UFUNDI LA MARKETI FC WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA TU YA MCHEZO WAO DHIDI YA MADSON KUTOCHEZWA LEO HII....

Katika hali isiyotegemewa na Mashabiki wa Manispaa ya Lindi waliokuwa tayari wamejiandaa kushuhudia Mtanange wa Ligi Daraja la Tatu kati ya Madson FC (mtama) Vs Market Place Fc (Lindimjini) uliopangwa kuchezwwa leo hii katika Dimba la Ilulu, wameshindwa kufika uwanjani.

Awali timu hizo zote mbili zilihudhuria Pre Match majira ya saa nne asubuhi, lakini katika hali isiyotarajiwa Timu hiyo haikuweza kutokea uwanjani kushindana na Timu hiyo ya Market Place ambayo hivi sasa Tayari imesha jikusanyia Point 10 na kuifanya kuwa timu ya Kwanza kukata tiketi ya kuendelea na ligi hiyo katika hatua ya Mzunguko unao fuata ambapo zitakutanishwa Timu nne, Mbili za Lindi na Mbili za Nachingwea ili kutafuta Bingwa atakae panda Ligi daraja la Pili.

Kesho katika Muendelezo wa Kumsaka nani atakae ungana na Timu ya Market Place zitakutanishwa timu za Beach Boys Vs Tranporter Fc (kilwa), Mchezo ambao unatazamwa kuwa wa ushindani wa hali ya juu kwani Timu zoto hizo mbili zinanafasi ya Kusonga mbele iwapo moja wapo itamshinda mwenzake.
Madson Fc Vs Market FC
Wachezaji wa Market Place wakipasha misuli huku waakiisubiri timu ya Madson Fc kutoka Mtama kuwasili uwanjani hapo..... 
Madson Fc Vs Market FC
Waamuzi wakipasha misuli huku wakiisubiri timu ya Madson Fc kutoka Mtama kuwasili uwanja wa Ilulu kwa Mchezo dhidi ya Market Place.... 
Madson Fc Vs Market FC
Benchi la Ufundi la Timu karibishwa likiwa wazi Baada ya Timu ya Madson Fc Kutoka Mtama kushindwa kufika kiwanjani..... 
Madson Fc Vs Market FC
Fourth Official akiteta jambo na Mchezaji na Shabiki wa Market Place baada ya Mechi kushindwa kuchezwa kwa sababu ya Timu ya Madson Fc kushindwa Kutokea Uwanjani...... 
Madson Fc Vs Market FC
Refa wa mchezo wa Leo akiongeea na Kaptani wa Timu ya Market Place Kuhusiana na Maamuzi ya Mchezo huo uliotegemewa kuchezwa leo hii na kushindwa kuchezwa kutokana na Timu ya Madson Fc kushindwa Kutokea Uwanjani. 
Madson Fc Vs Market FC
Wachezaji wa Market Place wakipiga dua mara baada ya Kumaliza Mzunguko huu wa kwanza wa Ligi Daraja la Tatu kwa kuwa Vinara wa Kituo cha Lindi na Kusubiri Hatua inayofuata kukipiga na timu zitakazo fanikiwa kupita katika Kituo cha Wilaya ya Nacchingwea. 
Madson Fc Vs Market FC
Mashabiki akina dada wa Timu ya Market Place wakiwa wamependeza na Jezi zao wakisubiri mchezo kati ya Madson Fc na Market Place ambao mchezo huo ulishindwa kuchezwa kutokana na Madson Fc kushindwa Kutokea Uwanjani.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top