LIGI KUU ENGLAND: JONJO AITUNGUA SOUTHAMPTON NA KUIBAKISHA MAN UNITED NAFASI YA 3!!

KIGONGO cha Mita 25 cha Dakika ya 83 cha Jonjo Shelvey, Mchezaji wa zamani wa Liverpool, kiliwapa ushindi wa Ugenini huko Saint Mary Swansea City walipoichapa Southampton Bao 1-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.

Ushindi huo umeipandisha Swansea hadi Nafasi ya 9 kwenye Ligi na kuhakikisha Southampton inabaki Nafasi ya 4 ikiwa Pointi 1 nyuma ya Manchester United.
Southampton pia walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Ryan Bertrand kumchezea Rafu mbaya Modou Barrow na kutolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 89.

VIKOSI: Southampton: Forster, Clyne, Fonte, Yoshida, Bertrand, Reed, S. Davis, Ward-Prowse, Tadić, Elia, Pellè

Akiba: K. Davis, Gardos, Mané, Targett, Seager, Gape.

Swansea: Fabianski, Naughton, Fernandez, Williams, Taylor, Fulton, Carroll, Shelvey, Dyer, Emnes, Gomis

Akiba: Tremmel, Rangel, Amat, Barrow, Tiendalli, Oliveira, Grimes.

Refa: Michael Oliver

MATOKEO: Jumapili Januari 18
Arsenal 5 Aston Villa 0

Southampton 0 Swansea 1 

MSIMAMO WA LIGI KUU YA UINGEREZA KWA SASA:-

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post