
Benchi la Ufundi la Timu ya Tranporter (kilwa) leo hii katika Mechi dhidi ya Beach Boys ambayo ilivunjika kutokana na vurugu kutokea...

Benchi la Ufundi la Timu ya Beach Boys leo hii katika Mechi dhidi ya Transporter (kilwa) ambayo ilivunjika kutokana na vurugu kutokea...

Waamuzi waliochezesha Mchezo wa Leo kati ya Beach Boys Dhidi ya Transporter Ndani ya Uwanja wa Ilulu katika Ligi ya Daraja la Tatu.
Na.Mwandishi Wetu, Lindi
Ligi Daraja la tatu Imemalizika leo hii Ndani ya Uwanja wa Ilulu Huku ikiingia Dosari ya Mchezo baina ya Beach Boys Vs Transporter Kuvunjika.Mechi hiyo Ilitawaliwa na Vurugu hasa katika Kipindi cha Pili wakati Transporter ikiwa Mbele kwa Magoli 3 - 0, Zilizopatikana Kipindi cha Kwanza kupitia Mfungaji Samuel Mtanda aliyepachika mabao yote Matatu Dakika ya 24, 27 na 41.
Kipindi cha Pili Timu ya Beach Boys Ilionekana Kubadilika na Kuishambulia Timu pinzani na Kubahtika kupata goli la Kwanza, Baada ya Kupata Goli hilo hapo ndipo kizaa zaa kilipoanza Wachezaji wa Transporter walionekana Kupaniki kwa mara nyingi kupinga maamuzi ya mwamuzi wa Kati na Kusababisha Mchezaji wao Mmoja kupewa kadi Nyekundu nakubaki pungufu.
Beach Boys waliendeelea kutumia nafasi hiyo na kujipatia Bao lingine la Pili Hapo hali ikazidi kuwa mbaya kwa Transporter lakini hawakukata tamaa na wakaendelea kucheza mpira.
Jambo ambalo lilipelekea Mpira Huo Kuvujika Nipale Mawasiliiano ya waamuzi kuwa hafifu hii ni baada ya Mwamuzi wa pembeni kushindwa kuwa na Msimamo katika maamuzi yake kwani Alionesha kibendera juu ikiwa anamaanisha ni Offside, Kipa alichokifanya ni kuutenga mpira huo katika sehemu ya Mchezaji alipootea kabla hajapiga Mchezaji wa beach Boys alichokifanya ni kuupiga mpira huo wavuni na Refa bila hiana akaweka Kati mpira kuashiria ni Goli.
Kufuatia kadhia hiyo wachezaji wa Transporter hawakuweza kuvumilia na kuweza kumfuata Mwamuzi huku wengine wakimfuata Kibendera na yeye hakuchelewa alitoka mbio hadi kati vyumba vya Kubadilishia nguo. na hapo ndipo Askari walipoingilia kati kuanza kufyatua Mabomu ya machozi kwa ajili ya kuwatawanya mashabiki walioanza kuingia uwanjani.
Hadi Tunatoka uwanjani hapo Mpirahuo haukuwezwa kumalizwa na Mwamuzi. Chama Cha Mpira cha Lindi kinatarajia kufanya kikao siku ya Kesho kujadili hatma ya Mchezo huo.
Kufuatia kutotokea katika Mchezo wao wa Mwisho timu ya Madson Fc imepelekea kufutwa michezo yao iliyochezwa awali katika Ligi hiyo hivyo kufanya Timu ya Transporter kama Mechi hiyo ingemalizika kwa Matokeo hayo ya 4 - 3 ingekuwa imetolewa katika mashindano hayo.

Mashabiki wa Timu ya Beach Boys wakishangilia mara baada ya Kupata Goli la Kusawazisha ambapo awali walikuwa wametulia kama maji mtungini.....

Mwamuzi akimuonesha kadi Nyekundu mchezaji wa Transporter baada ya Kufanya madhambi.....

Wachezaji wa Transporter wakimsihi mwenzao Kutoka Uwanjani Baada ya Kupewa Kadi Nyekundu na mwamuzi wa Mchezo huo...

Askari wakiingilia Kati kuwadhibiti wachezaji wa Transporter ambao walikuwa wakimzonga Mwamuzi mara baada ya Kufungwa Goli la 4 lenye Utata....

Askari waliongezeka Uwanjani hapo Kuhakikisha Usalama Unapatikana....

Wadau wa Mpira wakiwa wanastajabu kinachoendelea Uwanjani hapo hii ni Mara baada ya Mabomu ya Machozi kupigwa Uwanjani Hapo...

Mh. Mbunge wa Kilwa Kusini Suleiman Saidi Ally Bungala "Bwege" akiwasihi Mashabiki na viongozi wa Timu ya Transporter kuwa watulivu ili kujua hatma ya Timu yao.

Wamuzi waliweza kutoka Uwanjani hapo kwa Eskoti ya Gali la Polisi kwa ajili ya Usalama wao....
Tags
SPORTS NEWS