BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)

NOTISI YA SIKU 30 YA KUSUDIO LA KUFUTA USAJILI NA KUSHUSHA HADHI YA
USAJILI KWA VYUO/TAASISI ZA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Notisi
Kwa kutumia Sheria na Kanuni za Baraza [National Council for Technical Education (Registration of Technical Institutions) Regulations, 2001 na National Council for Technical Education (Accreditation and Recognition of Technical Institutions) Regulations, 2001 Baraza linatangaza kwamba linatoa notisi ya siku 30 kwa vyuo/taasisi ziilizokiuka taratibu za Usajili na Ithibati zifuatazo:
a) Vyuo/Taasisi ambazo muda wake wa Usajili wa Awali na Usajili wa Muda umekwisha;
b) Vyuo/Taasisi ambazo zimepitisha muda wa kuanza mchakato wa Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; na
c) Vyuo/Taasisi ambazo muda wake wa Ithibati umekwisha.
Vyuo/taasisi ambazo zinapewa notisi ni kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali Na. 1 na Na. 2.
Tags
HABARI ZA KITAIFA