DAR YOUNG AFRICANS (YANGA) KUIFUATA BDF XI YA BOTSWANA KESHO KUTWA

Dar Young Africans
Na Iblahim Karimu,Dar es Salaam.
KIKOSI kamili cha Dar Young Africans kinatarajia kukwea pipa kesho alfajiri kuelekea Botswana tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya BDF XI ya huko.

Katibu wa Yanga,Dr Jonas Tiboroha amesema kikosi chao kitaondoka na wachezaji wote watakao pitishwa na Kocha wao Hans Pluijm ambaye kesho atataja idadi kamili ya msafara wao.

Tiboroha ambaye kitaaluma pia ni kocha amesema kikosi chao kitaondoka na ndege ya shirika la Kenya tayari kwa mchezo huo wa kombe la shirikisho utakao pigwa Ijumaa nchini humo ambapo Yanga itarejea Jumapili baada ya mchezo huo.

"Tunatarajia kuondoka hapa Jumatano kesho kutwa kuelekea Botswana,kwa sasa tunasubiri kocha na timu irejee leo ikitokea Mbeya na baada ya hapo tutamaliza maandlizi ya Safari yetu,"amesema Tiboroha.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post