Unknown Unknown Author
Title: WOLPER ADAI HAWEZI KUANDIKWA BURE NA COCA COLA, AWATAKA WANASHERIA KULIANGALIA SUALA HILO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Katika Hali isiyo ya Kawaida Muigizaji Maarufu hapa Nchini Tanzania JACKLINE WOLPER amefunguka kuhusiana na Kampeni mpya ya Vinywaji Bari...
wolper na Coca cola
Katika Hali isiyo ya Kawaida Muigizaji Maarufu hapa Nchini Tanzania JACKLINE WOLPER amefunguka kuhusiana na Kampeni mpya ya Vinywaji Baridi ya Coca cola Kutumia Majina ya Mastaa wakubwa Nchini na Kuipa jina la #shareacokeTz Na.......

Msanii huyo amefunguka Kupitia account yake ya Instagram na Kuonyesha Masikitiko yake katika zoezi hilo ambalo yeye amelifananisha kama Uzalilishwaji kwani Kampuni hiyo Kubwa Barani Afrika ingeweza Kuwaita na kufanya makubaliano nao kisha kutekeleza Jambo hilo ili kuonesha kuwajali na Kuheshimu wadhifa wao Kwa jamii....


Ameitaka Serikali na wanasheria kuliangalia suala hili kama wanavyokemea wale wa wauza CD wa Kariakoo...

Hii ndio Post yake::
wolper na Coca cola
habari Followers pamoja na wa Tanzania wote ambao naamini huwa mnaingia katika page yangu ya insta.Nimepokea zawadi hii ya coca cola kwa siku 6 ,Na sio kwamba sikutaka kupiga picha kama wenzangu au ku post kama wenzangu ,nilikuwa natafakari Kweli Kampuni kubwa ya Kitaifa Na Kimataifa inaweza kutumia gharama kubwa kuandika majina Yetu bila kuchukuwa hata nafasi na heshima kubwa tuliyonayo kutushirikisha tu katika makubaliano ya kuandika majina Yetu Katika Makopo Yao.Maana Naamini maFan's wa woolper wangeweza kushare na coca cola kutokana Jina Langu kuwa label katika makopo yao.Sasa Naamini tuna wanaharakati,wabunge,wanaSheria pamoja na serikali ambao huwa wanafwatilia wale wauza CD wa kariakoo basi Naomba Juhudi hizi mzihamishie huku katika kampuni hii kubwa ya Kimataifa coca cola ili kutetea haki za Wasanii na sio kudhalilishwa kwa kiasi hiki jamani.sijui kama wasanii wenzangu walilipwa siwezi kuwasemea lakini haya ni mawazo yangu binafsi. #shareaCokeTz

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top