Unknown Unknown Author
Title: VIONGOZI WATATU WAKAMATWA SAKATA LA PANYA ROAD JIJINI DAR
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KILE kinachoonekana watu wameanza kuchoka na Vituko vyake pamoja na Visa anavyofanya Mtangazaji Maarufu wa redio ya Clauds Fm Eprahim Kib...
Kamishna Kova
KILE kinachoonekana watu wameanza kuchoka na Vituko vyake pamoja na Visa anavyofanya Mtangazaji Maarufu wa redio ya Clauds Fm Eprahim Kibonde, baada ya leo Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaa Kamishna Suleiman Kova kumjia Juu mtangazaji huyo na kumwambia aache utoto na kama anataka umaarufu atafute njia nyengine.

Kauli hiyo Kamishna Kova imekuja siku chache baada ya Mtangazaji huyo wa Kipindi cha Jahazi kujitokeza na kusema katika Vurugu zilizotokea mwishoni mwa wiki iliyopita zilizofanywa na Vijana wa Panya Road katika maeneo mbalimbali ya jiji hili,katika watu walikumbana adhia hiyo mtangazaji huyo alipata matatizo,baada ya kudai kupigwa na vijana hao.

Kalipio hilo la Kamishna kova ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na Waandishi Habari alipokuwa akilizungumzia sakata la Panya Road,ambapo pamoja na mambo mengine huku akizungumza pasipo kumtaja jina lakini tayari waandishi wa habari walikuwa wamegundua anamlenga mtangazaji huyo,alisema inasikitisha watu wanakuwa wanapotosha umma kiasi ambacho wangetakiwa kuwa wakweli kutokana na kazi wanazofanya za kutoa habari kwa jamii.

“Hivi mtu mwenye kama Yule tena maarufu sana na jamii inapenda kumsikiliza kwenye kipindi chake kupotosha watu kwamba panya road wamemvamia inashangaza sana,maana jeshi la polisi tumechunguza tumebaini akufanyiwa kitendo chochote kabisa, bali yeye anafanya hivyo huku akitaka umaarufu wakijinga”alisema Kamishna Kova.

Kamishna kova aliongeza kuwa jamii inahitaji watu kama hao kutoa taarifa za ukweli ila inasikitisha kuona wanataka umaarufu wa kijinga ambao hauna tija katika jamii kwani umaarufu aliokuwa nao unatosha kama mtangazaji huyo anataka kujilikana zaidi atafute njia nyengine.

Katika Hatua Nyingine Kamishna Kova aliwataja Viongozi wa watatu aliowakamata ambao walihusika katika kusimamia vitendo hivyo vya kiovu ambao ni Halfani Nurdini miaka 24,mkazu wa tandale Sokoni Jijini Dar es Salaam,Said Mohamed miaka 22 naye pia ni makazi wa Tandale,

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top