RONALDO AZIDI KUNG'AA KATIKA LALIGA, AFUNGA MAWILI HUKU REAL MADRID IKIICHAPA GATAFE 3 - 0

Real Madrid Vs Gatafe
Mabingwa wa ulaya , Real Madrid wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwafunga wapinzani wao toka jijini Madrid Getafe katika mchezo wao wa 18 wa ligi kuu ya Hispania .

Madrid walihsinda mchezo huo kwa matokeo ya 3-0 wakifunga mabao yao kupitia kwa Cristiano Ronaldo na Gareth Bale ambapo Ronaldo alifunga mabao mawili .

Ushindi huu unawafanya Real wafikishe idadi ya pointi 45 baada ya kucheza michezo kumi na nane .

Kwa upande wa Cristiano Ronaldo, mabao mawili aliyofunga hii leo yanamfanya afikishe idadi ya mabao 28 ambayo amefunga kwenye mechi 18 idadi inayomfanya aendelee kukaa kwenye kilele cha orodha ya wafungaji bora huku pia akiongoza orodha ya pasi za mwisho akiwa amesaidia pasi za mwisho kwa wenzie mara 9.

Real Madrid bado wana mchezo mmoja mkononi ambao utawafanya wafikishe idadi ya michezo 19 kama ilivyo kwa timu nyingine za ligi ya Hispania .

Real Madrid Vs GatafeMabao matatu dhidi ya Getafe yalifungw ana Ronaldo (2) na Gareth Bale (1)
Real Madrid Vs GatafeRonaldo anaongoza kwa kufunga magoli (28) na kwenye pasi za mwisho (9).

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post